Waendesha
Baiskeli Maarufu kwa jina la daladala wanaosafirisha abiria kwenye halmashauri
ya mji wa Geita, wamepinga agizo la Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo la kuwataka
kufikia leo wasitishe shughuli zao kwenye maeneo ya mjini badala yake wafanye
kwenye maeneo waliyopangiwa.
Hatua hiyo
imekuja baada ya kupewa muda wa siku tano kupisha maeneo ya mjini kutokana na
wimbi la ajali zinazosababishwa na waendesha Baiskeli kwa kutotumia barabara
vizuri wanapokuwa kwenye shughuli zao.
Baadhi ya
waendesha Baiskeli hao Bw Vistusi Maagani, John Maige na Fredy Maganga wamesema
utaratibu uliofanyika sio mzuri kwa kuwa hawajapewa maeneo yatakayowasaidia
kufanya kazi zao .
“Nasikitishwa
sanaa na kitendo cha Mkurugenzi kututoa bila ya kutuandalia maeneo mazuri ya
kufanyia kazi zetu kwa mfano mimi hapa hii kazi ndio nategemea kulisha familia
pia kutuma pesa kwa mama yangu mzazi kwa kuwa sina ndugu leo natolewa kufanya
kazi mjini unategemea nitaishi maisha gani jamani na wale ambao wananitegemea
nitawaelezaje mimi naomba haya maamuzi wayaangalie kwa umakini”Alisema Maagini.
“Nashindwa
hata niseme nini najisikia moyo wangu kutoka kabisa kutokana na taarifa hii ya kuondolewa
mjini maeneo ambayo tunaambiwa kufanya kazi akuna abiria sasa sijui tutaishije
sisi waendesha daladala”Alisema Maganga.
Bi,Lucia
Paul ambaye mume wake anajishughulisha na kazi hizo alisema kuondolewa mjini kwa waendasha baiskeli
kutaleta athari kwenye familia zao kutokana na wengi wao kutegemea shughuli
hiyo kukidhi mahitaji ya familia.
“Kwasasa
hivi nyumbani hapakaliki kila siku mume wangu anamawazo anashindwa afanye nini
na uku anafamilia muda mwingine hadi namuonea huruma serikali ni vyema ikaangalia maana itatupa
wakati mgumu sisi wanawake ambao tunawategemea waume zetu kwenye utafutaji”Alisisitiza
Lucia.
Kutokana na
hali hiyo chama cha ACT wazalendo kupitia kwa katibu wa mkoa huo,Bw Ikolongo
Otoo ameitaka halmashauri ya mji wa
Geita kuondoa mara moja zuio hilo kwa
kuwa ni la kibaguzi ambalo alijazingatia wala kuthamini vijana masikini na
wanyonge ambao wameamua kujipatia vipato kwa njia halali kabisa.
Mkurugenzi
wa Halmashari ya mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly alisema suala ambalo linafanyika ni la
utekelezaji na alilikuwa aliitaji muda
kwani maeneo ambayo wamewapatia kufanya biashara ni makubwa na kwamba hata
wangepewa muda wa kutosha bado
wangeombwa kuongezewa.
Mbunge wa
Jimbo la Geita mjini,Constatine Kanyasu alisema ahafikiani na makubaliano hayo na kwamba akuna
utaratibu wala sheria ambayo inawazuhia waendesha Baiskeli kufanya shughulo zao
maeneo ya mjini.
Post A Comment: