Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla wakati alipozuru ofisini kwake mara baada ya kuwasilia mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku, Leo 20 Februari 2018.
Picha ya pamoja Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (katikati) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla mara baada ya mazungumzo wakati alipozuru ofisini kwake akiwa mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, Leo 20 Februari 2018. Wengine pichani ni Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njenza CCM (Kulia), Katibu tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi Mariamu Mtunguja (Wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika (Wa kwanza kushoto).
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akisikiliza kwa makini taafifa kuhusu sekta ya madini kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla wakati alipozuru ofisini kwake mara baada ya kuwasilia mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku, Leo 20 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Mbeya
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ameanza ziara ya
kikazi katika Mkoa wa Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea kiwanda
cha kutengeneza Samani mbalimbali zinazotokana na Marble, kukagua shughuli za
uchakataji Madini ya malumalu na mradi wa Pandahili (Niobiaum).
Maeneo mengine atakayotembelea ni pamoja na mgodi wa Sunshine
uliopo katika Wilaya ya Chunya ambapo atazungumza pia na wachimbaji wadogo
katika migodi atakayotembelea.
Mara baada ya kuwasili katika Mkoa wa Mbeya Mhe Biteko amesifu
juhudi za Mkuu wa Mkoa huo Mhe Amos Makalla kwa uthubutu mkubwa katika utendaji
ikiwa ni pamoja na usimamizi madhubuti katika sekta ya Madini.
Pamoja
na pongezi hizo Mhe Biteko amemsihi Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya kuongeza juhudi
zaidi ili kutimiza ndoto ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt
John Pombe Magufuli kuwatumikia watanzania na kupelekea kunufaika na rasilimali
zao ikiwemo sekta ya Madini.
Alisema kuwa Sekta ya Madini bado ni muhimu hivyo inahitaji
kulelewa ili ikuwe na hatimaye kuongeza ufanisi katika uchangiaji wa pato la
Taifa
Alisema kila kiongozi ana wajibu mkubwa kuwa mbunifu katika
uwajibikaji wake huku akiongeza kuwa Jukumu la msingi la kiongozi ni pamoja na
kutafsiri ndoto za Rais Magufuli ili kuwafanya wananchi kunufaika na uongozi
bora na utendaji wa serikali ya awamu ya tano.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makala
amesisitiza kuendeleza ushirikiano madhubuti na Wizara ya Madini ili wananchi
Mkoani humo wanufaike na matunda ya kukichagua Chama Cha Mapinduzi kuongoza
dola.
Post A Comment: