Mwishoni mwa mwaka 2016 Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan alizindua mabweni ya kisasa ya wasichana katika shule ya sekondari Idetemya iliyopo wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Mabweni hayo yalijengwa na shirika la ASAP (Africa School Asistance Project) kutoka Marekani linalosaidia maendeleo ya elimu barani Afrika kupitia mradi wake wa Kupanda wenye lengo la kuhakikisha mazingira ya shule yanaboreshwa hususani kwa wanafunzi wa kike ili waweze kupata fursa ya kumaliza elimu.
Ungana nasi ili kujionea mabweni hayo mwanzo hadi mwisho na pia namna yalivyosaidia kuleta mabadiliko ya ufaulu katika shule hiyo ya Idetemya hususani kwenye ufaulu wa wanafunzi wa kike katika matokeo ya kidato cha nne.
Post A Comment: