Barabara ya mtaa wa Nshinde Kata ya Nyankumbu Wilayani Geita ikiwa imeharibika kutokana na mvua ambazo zinaendelea Kunyesha. |
Mwananchi akishindwa kupita na usafiri kwenye Barabara ambayo imeharibika kwa kiasi kikubwa. |
Mwenyekiti wa mtaa wa Shinde Bw,Makoye Mirambo akizungumza juu ya uharibifu huo unavyowaathiri wananchi wake. |
Na,Joel Maduka,Geita
Wananchi wa mtaa wa Nshinde Wilayani Geita wamelalamikia ubovu wa barabara inayoelekea fadhiri bucha na mwatulole kuwa kero kubwa kutokana na ubovu ambao umekuwa ukisababisha gari nyingi kukwama na kukosekana kwa baadhi ya huduma za usafiri.
Akizungumza na mtandao huu Bi Fatuma
mwita amesema tatizo hilo ni la muda
mrefu na bado halijapatiwa ufumbuzi
jambo ambalo linapelekea usumbufu katika harakati zao za kutafuta maendeleo na
kwamba wamekuwa wakipata shida pindi hususani mvua zinaponyesha.
Aidha ameongeza kuwa wamekuwa wanapata usumbufu mkubwa
kutokana na kuwepo mashimo katika barabara hiyo na kupelekea baadhi ya madereva
kukataa kupita na wengine Hali ambayo
imeendelea kusababisha kuendelea kuharibika kwa barabara.
“Inafika
wakati watoto wanashindwa kwenda shule kutokana na ubovu huu wa barabara jamani
yani huku sisi tumekuwa kama tupo kisiwani ambapo akuna huduma nzuri tunaomba serikali isikie kilio chetu
itusaidie”Alisema Fatuma.
Naye Bw,Emmanuel John alisema ubovu wa barabara
hiyo umechangia baadhi ya madereva
wa piki piki kushindwa kufika hata pindi
wanapokuwa na wagonjwa hivyo kujikuta wakipata shida kubwa zaidi kutokana na
ubovu huo.
Hata hivyo Diwani wa kata hiyo,Michael
Kapaya alikili kuwepo kwa ubovu wa
barabara hizo na kwamba kwa sasa bajeti za utengenezaji unafanywa na TARURA na
wamekwisha kuziingiza kwenye bajeti hivyo anatarajia muda wowote zitaanza
kujengwa.
Kaimu meneja
wa Tarura halmashauri ya mji Bw ILDEPHONCE ZIRIRA amesema ujenzi wa barabara unaenda kwa hatua
kwa hatua na kwamba wamekwisha pereka bajeti ya mwaka 2018 /19 hivyo anaamini mwaka huu zitajengwa kwenye maeneo
ambayo yanachangamoto kubwa ya uharibifu.
Post A Comment: