Wananchi na
watumishi pamoja na wale ambao wanafanya kazi sekta binafisi mkoani
Geita,wametakiwa kutumia fursa ya chuo kikuu huria kwaajili ya kuongeza kiwango
cha elimu pamoja na maarifa ambayo
yatawasaidia kwenye shughuli zao za kila siku.
Wito huo umetolewa na Waziri Mkuu mstaafu,ambaye ni Mkuu wa chuo kikuu huria nchini,Mizengo Pinda wakati wa ziara yake ya kutembelea na kujionea shughuli ambazo zinafanywa na chuo hicho mkoani humo pamoja na kuzungumza na wanafunzi.
Mh,Pinda alisema ni vyema kwa wakuu wa mikoa kuendelea kuhamasisha watumishi ambao wapo kazini kujiongezea uwezo zaidi kielimu kwenye vyuo vikuu huria ili kufikia adhima ya Tanzania ya viwanda ifikapo 2025.
“Mkuu wa mkoa na katibu tawala tusaidie sanaa kuhamasisha kundi la watalaamu ambao wapo serikalini kutumia fursa hii kujiongezea uwezo hili waweze kuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kielimu”Alisisitiza Pinda.
Naye mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema suala la elimu alina
mwisho kwani pindi unavyozidi kuongeza
elimu ndio unafungua mianya ya kukabiliana na janga la umasikini.
“Elimu aina
mwisho jinsi ambavyo unachukua nafasi ya kupata elimu unapata uwezo wa kupigana
vita vya umasikini vita vya kuondoka kiwango ulichopo kwenda kwenye kiwango cha
juu hivyo basi natoa wito kwa wananchi wote waliopo mkoa wa Geita watumia fursa
hii kujiendeleza kielimu kwenye chuo hiki huria”Alisema Luhumbi.
Hata hivyo mkurugenzi wa chuo kikuu huria tawi la Geita,Ally Abdul,ameishukuru serikali
kwa kuwapatia hati miliki ya kiwanja kwaajili ya kuongeza majengo pamoja na msaada wa
vitabu 285.
Chuo kikuu
huria Tawi la Geita kilianza mwaka 2012
na kufanya kazi rasmi mwaka 2013 kikiwa na takribani ya wanafunzi 74 na wengi
kati ya hao walisajiliwa kutoka Mwanza
wakati huo Geita ikiwa ni wilaya hadi ya
wanafunzi iliongezeka kwa mwaka 2014 na 2015 kufikia idadi ya 118 na mwaka huu jumla ya
wanafunzi ni 285.
Post A Comment: