Wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri mbili ya mji na wilaya ya Geita wakisaini makubaliano.(katikati) Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM) Bw. Richard Jordinso. |
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi aweka saini kwenye hati ya makubaliano ya miradi kwenye halmashauri mbili ya mji na wilaya. |
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akimkabidhi hati ya makubaliano mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola. |
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi ,akimkabidhi hati ya makubaliano mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita,Elisha Lupuga.
NA,JOEL MADUKA,GEITA.
|
Kampuni ya Geita
Gold Mining Limited (GGM) pamoja na Halmashauri
mbili za Wilaya na Mji wa Geita zimetia saini ya Makubaliano ya Ushirikiano wa pamoja
kuhusu Matumizi ya fedha za Huduma za Jamii zinazotolewa na Kampuni hiyo kwa mwaka
2018.
Saini ya Makubaliano
hayo inafuatia kutokana na marekebisho ya Sheria Mpya ya Madini iliyopitishwa na
Serikali ya Tanzania kwa lengo la kufanya mageuzi kwenye utekelezaji wa Fedha za
Miradi ya Huduma za Jamii baina ya Kampuni za Uchimbaji Madini na Jamii kwenye eneo
husika.
Mkuu wa Mkoa
wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema Serikali mkoani humo imekusudia
kuanzisha miradi mipya ikiwemo kiwanda cha sukari kutokana na mapato
yanayotolewa na mgodi wa dhahabu wa GGM baada ya kuingia mkataba upya na
halmashauri ya mji na wilaya ya Geita.
Aliongeza
kuwa fedha zilizokwisha kutolewa na GGM kwa mwaka huu ni Bilioni tisa pointi
mbili (B 9.2) ambapo fedha hizo zitatumika kuanzisha miradi mbalimbali itakayo
wawezesha wananchi kujikwamua na umasikini, ikiwemo kiwanda cha sukari ,afya
elimu na mazingira.
“Kifungu cha
105 (01) cha Sheria Mpya ya Madini kinazielekeza Kampuni zote za Uchimbaji Madini
kuandaa Mpango wa matumizi ya Fedha za Huduma ya Jamii kwa kushirikiana na Halmashauri
husika kabla ya kuanzisha Miradi yoyote ya Maendeleo,na hiyo ndiyo sababu leo hii
makubaliano hayo ya nafanywa,” alisema Luhumbi.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM) Bw. Richard Jordinso alisema kuwa wanajivunia
mafanikio hayo na kwamba wanaamini kufanya kazi na jamii inayowazunguka ili
kuweza kuleta chachu ya maendeleo kwenye jamii inayouzunguka mgodi huo.
Makubaliano hayo ambayo yamefikiwa jana yatatarajia kutekeleza miradi mipya ya maendeleo kwa mwaka
2018 katika sekta ya afya ,miundo mbinu,mjai,elimu,sanaa na utamaduni pamoja na
kuwajenhea uwezo wajasiriamali wadogo na wakati.
Post A Comment: