Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale Mhe Hussein Nassor Amari Kasu akizungumza na kuelezea kero ambazo wamekuwa wakizipata wachimbaji wadogo za kuondolewa kila mala kwenye maeneo ambayo wanayazindua. |
Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale Hamim Gweyama akiwaeleza wachimbaji kufuata taratibu na sheria ambazo zimewekwa kwenye maeneo ya uchimbaji madini. |
Na,Joel Maduka,Geita.
Serikali
imesema imedhamiria kuwanufaisha wananchi kupitia rasilimali za nchi hususani
sekta ya Madini hivyo wachimbaji wadogo wanapaswa kuzingatia maelekezo ya
serikali ikiwemo taratibu na sheria katika uchimbaji.
Naibu Waziri
wa Madini Bw DotoBiteko ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wachimbaji
wadogo katika Kijiji cha Bululu, kilichopo Kata ya Nyamtukuza Wilayani
Nyang'hwale Mkoani Geita.
Alisema Serikali
imetenga maeneo maalum kwa wachimbaji wadogo katika mkoa wa Geita na maeneo
mengi nchini huku akisisitiza kuwa kuna leseni za utafiti na uchimbaji mdogo 24
ambazo zinaisha muda wake March 30 mwaka huu katika Wilaya ya Nyang'hwale.
Amewataka
wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kwa kuwa Serikali inatazama namna
ya kuwapatia wachimbaji wadogo baadhi ya maeneo hayo.
Naibu waziri
Biteko ameendelea kusema kuwa serikali
itatoa leseni kwa ajili ya maeneo ya uchimbaji lakini haitatoa leseni hizo kwa
mtu mmoja mmoja badala yake amewasihi wachimbaji hao kuanzisha vikundi ili
kupatiwa leseni hizo.
Mbunge wa
Jimbo la Nyang’hwale Bw Hussein Kasu alimueleza Naibu waziri kuwepo kwa tabia ya kufukuzwa wachimbaji wadogo hata kama wanakuwa
wakivumbua maeneo ambayo yanadhahau kwa madai kuwa yapo ndani ya leseni hali
ambayo imewapelekea kujiona kama wao ni wakimbizi.
Hata hivyo
kufuatia agizo ambalo limetolewa na Naibu waziri wa madini Bw Biteko, baadhi ya
wachimbaji wamesema matarajio yao yalikuwa ni kuruhusiwa kuendelea kufanya kazi
kwenye maeneo ambayo walikuwa wameanza
uchimbaji hivyo hawaafiki kuendelea kusubilia hadi tarehe ambayo
wameambiwa .
Aidha Biteko pia amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya
Nyang'wwale Bw Hamim Gwiyama kuitisha kikao ndani ya wiki moja kwa kuwaalika
wananchi wote wenyewe vikundi ili kuwaelekeza namna bora ya kufanya kazi za uchimbaji
kwa kufuata taratibu na sheria.
Post A Comment: