Wanafunzi wa
shule ya msingi Mchongomani kata ya Katoro mkaoni Geita wanasomea nje wakiwa wamekaa chini na wengine
kubanana kwenye madawati kutokana na
shule hiyo kukabiliwa na Upungufu wa madawati na vyumba vya madarasa.
Baadhi ya
wanafunzi hao Jesca Michael na Hoja Hassan wamesema hali hiyo imekuwa ikisababisha utoro kwa baadhi ya
wanafunzi na kwamba mvua zinaponyesha wamekuwa wakisitisha masomo.
“Tumekuwa
tukipata shida kubwa sanaa kusomea nje hali hii imekuwa ikisababisha baadhi ya
wanafunzi wenzetu kushindwa kuja shule kutokana na haya mazingira ya kusomea
nje”Alisema Jesca.
“Tunaathirika
sanaa macho kusomea nje kwani muda mwingine jua likiwa kali limekuwa
likituumiza macho na siku nyingine mvua zikinyesha uwa tunashindwa kusoma hali
hii imekuwa ikisababisha kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo yetu tunaomba
serikali itusaidie kwani tunateseka sanaa hadi muda mwingine tunawaonea huruma
walimu wetu."Alisema Hoja.
Kwa upande
wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw Faustine Makulu amekili kuwepo kwa tatizo la uhaba wa vyumba
vya madarasa na kwamba uhitaji wa vyumba vya madarasa ni 46 na kwasasa
wamejenga vyumba 4 na vinavyotumika ni viwili huku wanafunzi waliopo shuleni
hapo ni 2072.
“Hapa
shuleni kwangu hali siyo nzuri pamoja na jithada ambazo zimeendelea kufanywa na
serikali lakini uhitaji ni mkubwa sanaa ukilinganisha na watoto waliopo na
madarasa ambayo yapo utaona hali ilivyo kiuweli hadi sasa hivi jitihada ambazo
zinaendelea ni ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa”Alisema Mwalimu Makulu.
Aidha Mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya ya Geita, Bw Ali Kidwaka alisema wanafanya jitihada za kujenga vyumba vya
madarasa 322 wilayani humo vikiwemo katika shule hiyo na kwamba wanatarajia
kufikia Desemba mwaka huu wawe wamepunguza changamoto ya upungufu wa madarasa.
Post A Comment: