Shekhe Yusufu, akiwaeleza waumini namna ambavyo wanatakiwa kuendelea kumcha Mungu na mwisho wa siku ni vyema wakafika katika Nchi ya Saud Arabia kwaajili ya kuhiji.
Waumini wakimsikiliza kwa makini shekhe wakati wa ibada ya shukrani.
GEITA:Mahujaji
wanne wakiongozwa na Shekhe Mkuu wa Mkoa
wa Geita,Alhadi Yusufu Kabaju,wamerejea mkoani humo wakitokea nchini Saud Arabia ambako walikwenda kuhiji ikiwa ni moja kati ya nguzo muhimu
katika Dini ya Kiislamu.
Akizungumza
katika ibada ya kumshukuru Mungu kuwarudisha salama,shehe Alhadi Yusufu Kabaju,amesema
kuwa ni jambo la busara sana kumshukuru Mungu kwani amewasaidia katika safari yao kwenda na
kurudi salama.
“Ni jambo la
kumshukuru mwenyezi Mungu sana na Mtume wake
Muhammad (SAW) ni jambo ambalo waislamu
tunapaswa kumshuru mwenyezi Mungu sana ,safari ya kiibada ni safari nzito sana
kwasababu ukiangalia safari ya kwenda na kurudi ni safari nzito sana huwezi
ukaamini kuwa mtu anaweza kwenda safari hiyo na umma wa Dunia nzima mkakutana
sehemu moja.”alisema Shehe Kabaju.
Aidha kwa
upande wao wahumini wa dini ya kislamu wameshukuru na pia wamefurahia kwa
kurudi salama kwa mahujaji ambao walikwenda kuhiji Makkah.
Mahujaji hao wamerejea siku ya Jumamosi wakitokea nchini
Saudi Arabia ambako walikwenda kuhiji.
Imeandaliwa
na Joel Maduka.
|
Post A Comment: