PICHA NA MATUKIO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARA BARANI MKOANI GEITA

Share it:
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni, akiwasili katika viwanja vya kalangalala Mkoani Geita huku akipokelewa na makamanda wa Jeshi la Polisi Nchini.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akisalimiana na moja kati ya watu wenye ulemavu wa viungo katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama.


CPL Faustina Ndunguru kutoka Traffik makao makuu akitoa maelekezo mbele ya mgeni rasmi katika banda la maonesho la kikosi cha usalama barabarani.

Traffik Devid Kasembe akitoa maelezo juu ya kifaa cha malipo pindi wanapowakamata wale  ambao wanakwenda kinyume na  sheria ya usalama barabarani.







Maandamano yakiingia katika viwanja vya kalangalala.





Akitoa taarifa ya Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani,Kamanda  wa kikosi cha usalama barabarani Nchini ,Mohamed Mpinga mbele ya mgeni Rasmi.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekieli  Kyunga,akishukuru  kwa Baraza la Taifa la usalama barabarani kufanyia Maadhimisho ya wiki ya nenda  kwa usalama barabarani mkoani Geita .


Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekieli  Kyunga,akikabidhiwa cheti cha ushiriki wa wiki ya nenda kwa usalama na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi  Hamad Masauni.



Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo akipokea cheti cha ushiriki.

Afisa Rasilimali watu wa Kampuni ya Puma Loveness Hoyange akipokea cheti cha ushiriki,baada ya kufanya vizuri katika kudhamini mashindano ya wanafunzi kuchora alama za barabarani.

Mkurugenzi wa mawasiliano na uhusiano wa vodacom Tanzania Rosalynn Mworia akipokea cheti cha ushiriki wa kampuni ya vodacom.

Meneja masoko wa Selcom Tumain Mgori ambao ni wawezeshaji wakuu wa malipo ya mtandao kwa kutumia kadi na huduma za kibenki,pia ni wasambazaji wa mashine za Point of sale ambazo zinatumika kuuza Luku ,vocha na malipo mbali mbali akipokea cheti cha ushiriki.

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi cheti cha ushiriki, Mwakilishi wa Kampuni ya Bia nchini (TBL), Amanda Walter

Neema Swai,kutoka Kampuni ya Puma akifafanua juu wao kushiriki katika utoaji wa zawadi.


Naibu  waziri  wizara ya Ujenzi  uchukuzi na mawasiliano   Mhandisi  Edwin Ngonyani ambae ni Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani nchini,amefafanua kuwa pamoja na jitihada ambazo zinafanywa na serikali bado kuna tatizo kubwa la madareva na wapanda pikipiki kutokujali sheria za usalama barabarani






 GEITAMaadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yamezinduliwa rasmi  leo ,Mkoani Geita katika viwanja vya kalangalala  na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi  Mhandisi Hamad Yussuph Masauni,huku ajali za waendesha piki piki maarufu boda boda zikiendelea kushika kasi kubwa  zaidi nchini.

Akitoa taarifa ya Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani,Kamanda  wa kikosi cha usalama barabarani Nchini ,Mohamed Mpinga,amesema kuwa Baraza la Taifa la Usalama barabarani  limekuwa na mikakati mbali mbali ya kukabiliana na ajali ambazo zimekuwa zikijitokeza hususani  zile ambazo zinachangiwa na uzembe barabarani.

“Baraza la Taifa la usalama barabarani Tanzania likishirikiana na jeshi la Polisi nchini  kupitia kikosi cha usalama barabarani pamoja na wadau wengine wa usalama barabarani limekuwa na mikakati mbali mbali ya kukabiliana na ajali za barabarani hapa nchini vyanzo  vya ajali vilivyopewa kipa umbele zaidi ni zile za makosa ya kibinadamu ambazo zinachangia takribani asilimia 80% ya vyanzo vyote vya ajali barabarani”.Alisema  Mpinga

Kwa upande wake Naibu  waziri  wizara ya Ujenzi  uchukuzi na mawasiliano   Mhandisi  Edwin Ngonyani ambae ni Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani nchini,amefafanua kuwa pamoja na jitihada ambazo zinafanywa na serikali bado kuna tatizo kubwa la madareva na wapanda pikipiki kutokujali sheria za usalama barabarani.

Aidha mgeni rasmi katika  Maadhimisho hayo Mh, Mhandisi Masauni ,amemtaka kila mtumiaji wa barabara kupambana kwa nguvu zote  katika kutokomeza ajali za barabarani na kwamba wajibu huo sio wa serikali tu bali wananchi nao wanahusika huku akitaja idadi ya ajali zilizotokea kwa mwaka huu.

“Nyingi za ajali zinazotokea ni kutokana na uzembe wa madereva  na kundi linaloongoza kwa kuathirika ni abiria ambapo kumekuwepo na vifo 3,444 na majeruhia 20,181 huku watembea kwa miguu vifo vikiwa ni  3,328 na waliojeruhiwa ni 8,256 kutokana na ajali za barabarani lakini kwa upande wa pikipiki ambao wanachukua nafasi ya tatu kwa vifo 2,463 na majeruhi 10,702, wakati wapanda baiskeli waliofariki ni 1,071 huku majeruhi wakiwa ni 2,060 madereva waliofariki jumla ni 813 wakati waliojeruhia ni 3,157.”Alisema Masauni.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekieli  Kyunga,ameshukuru kwa Baraza la Taifa la usalama barabarani kufanyia Maadhimisho ya wiki ya nenda  kwa usalama barabarani mkoani Geita akiamini kuwa ni moja kati ya njia ya kuutangaza Mkoa wa Geita.



Share it:

habari

Post A Comment: