NI AIBU KUIHOFIA MWADUI FC YA JULIO ,CANAVARO.

Share it:











Nahodha wa Yanga,Nadir Haroub 'Canavaro'
NAHODHA WA YANGA,NADIR CANAVARO.


Nahodha wa mabingwa watetezi Yanga,Nadir Haroun ‘Canavaro’ametamba kuwa hakuna namna lazima wapate pointi sita katika Ardhi ya Shinyanga na kuanza na mchezo wa Kesho dhidi ya matajiri wa Mwadui uwanja wa Kambarage Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Canavaro amesema kuwa ni dhambi kuilinganisha Mwadui na sisi kwani tumeweze kucheza na timu kubwa Afrika kuliko hii timu ya Kocha mwenye maneno mengi najua kesho baada ya kumshushia kichapo atakuwa na visingizio vingi hivyo tumejipanga kushinda mchezo wetu dhidi ya Mwadui.
“Mchezo wetu na Mwadui utakuwa kama fainali kwetu na tutacheza kufa na kupona ili tuweze kuondoka na pointi tatu kwani msimu uliopita tulitoka nao sare kutokana na uwanja kuwa ulikuwa na maji hivyo kipindi hiki hakuna Mvua japo uwanja si rafiki ndio maana tumejipanga ukizingatia tulikuwa tunafanya mazoezi katika uwanja wa Kaunda sababu ni mbovu kama wa Kambarage”alisema Canavaro.



Aidha Canavaro amesema kuwa hata kocha Mkuu Hans Van Der Pluijm amewapa mbinu za kucheza viwanja vya mikoani na pia ameshayafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo wetu ambao tulicheza ugenini na Ndanda tulilazimishwa sare ya bila kufungana hivyo tunashukuru baadhi ya wachezaji wetu wamerudi ambao walikosekana katika michezo yetu miwili.
Yanga wanategemea kucheza na Mwadui mchezo unaotabiriwa kuwa na upinzani wa aina yake kutokana na matajiri hao wa Mwadui wanafundishwa na Kocha Mkuu Jamhuri Kihwelu Julio ambaye ni mwanachama wa Simba hivyo inatafasiriwa kuwa yeye ana mapenzi na Simba na atawakazia Yanga kuibuka na ushindi siku ya kesho.



TAZAMA MECHI NYINGINE AMBAZO ZITACHEZWA WIKENDI HII.
JUMAMOSI SEPTEMBA 17:
.Mwadui FC vs Yanga
.Mbeya City vs Prisons
.Mtibwa Sugar vs Kagera Sugar
.Azam FC vs Simba
.Ruvu Shooting vs Mbao FC
.Majimaji vs Ndanda FC.
JUMAPILI SEPTEMBA 18:
.African Lyon vs Toto African

.Stand United vs Jkt Ruvu.



Share it:

michezo

Post A Comment: