PIKIPIKI 31 ZENYE THAMANI YA MILIONI 806,00,000 ZIMETOLEWA KWA MAKATIBU WA CCM WILAYANI CHATO.

Share it:
Pikipiki zilizotolewa zikiwa zimepakiwa
Katibu wa CCM kata ya buziku,Bahati Mayengera.


 Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa (NEC),Deodedisi Katware
Mnec akifafanua jambo na wajumbe.

Wajumbe wakifatilia kwa makini maagizo ya Mnec.


Bw,Katware akikabidhi pikipiki kwa viongozi.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama akijaribia kuwasha moja kati ya pikipiki.


Jumla ya pikipiki 31 zenye thamani ya milioni 806,000,000  zimetolewa kwa makatibu wa Chama cha mapinduzi (CCM)ngazi ya vitongoji ,vijiji na kata wilayani chato mkoani geita lengo likiwa ni kuakikisha wanaimalisha chama kwa kuraisisha utendaji wa kazi.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa (NEC),Deodedisi Katware,wakati wa zoezi la ugawaji wa usafiri huo,ambapo alisema  kuwa kutokana na kwamba kwa sasa kumekuwepo na ushindani wa kisiasa wanaamini kuwa kuwapatia pikipiki hizo zitasaidia kufanya kazi zao kwa wepesi na kuwatumikia wananchi kama ambavyo walihaidi kuwatumikia kwenye uchaguzi wa mwaka jana.

”Lengo kubwa la kutoa usafiri kwa viongozi wa chama ngazi ya kata kwa maana makatibu kwanza ni kuimalisha na kukiendeleza chama na tunatamani viongozi hawa wa ngazi ya kata watekeleze majukumu yao kama inavyotakiwa”alisema katware.

Akizungumza kwa niaba ya makatibu ambao wamepatiwa pikipiki hizo,katibu wa ccm kata ya Buziku,Bahati Mayengera,alisema kuwa kipindi cha nyuma wakati hawajapatiwa usafiri huo walikuwa na changamoto kubwa ya kutembea umbali wa kilomita nyingi kwaajili ya kwenda kutoa huduma kwa wananchama ambao wana maitaji.

“Kipindi cha nyuma wakati hatujapewa usafiri huu tulikuwa na shida sana hasa wakati wa kapeni na shughuli zingine za chama lakini kwa sasa kwa kuwa tumepatiwa usafiri huu tunaamini utatusaidia kuondoa usumbufu wa kutembea kwa baskeli.”Alisema Mayengera

Pamoja na kumpongeza kiongozi wa NEC,viongozi hao wamewaomba viongozi waliopo ngazi ya Taifa kuwakumbuka wale ambao wapo chini kwa kuiga  mfano huo na kuwa na moyo wa kutoa kama ambavyo amefanya bw katware kwani ngazi ya kata na vijiji wamekuwa wakisahaulika sana hali ambayo inapelekea kudhorotesha utendaji kazi wa chama.

Imeandaliwa na Madukaonline.


Share it:

habari

Post A Comment: