TAMASHA LA KUOMBEA AMANI KUFANYIKA JUMAMOSI JIJINI MWANZA

Share it:



Mwimbaji wa nyimbo za injili Gideon Musa,anayetarajia kufanya uzinduzi Jumamosi hii.








Lile tamasha kubwa la kuombea amani ambalo limekuwa likifanyika mkoani Mwanza linatarjia kufanyika jumamosi hiI katika uwanja wa ccm kirumba.


Akizungumza na mtandao wa madukaonline Mwandaaji wa  tamasha la amani Fabian Fanuel amesema maandalizi yamekamilika ambapo watu wengi wakiwemo watumishi wa Mungu na waimbaji mbalimbali wamepewa mwaliko wa kuhuduma katika hilo.


Fanuel amesema katika tamasha hili pia watawaombea watu waliopatwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera na uzinduzi wa albam ya Africa yake Gideon Musa utafanyika siku hiyo.


" tumejiandaa sana maana wananchi wameitikia  kuwepo katika tamasha hilo, Kwaya, Bendi na waimbaji binafsi ambao ni wakali wamethibitisha kushiriki katika tamasha hilo".Alisema Fabian


Tamasha hilo litafanyika jumamosi  katika viwanja vya ccm kirumba kuanzia saa sita mchana hadi kumi na mbili huku mlangoni watu wakitoa sapoti ya 1000/= kwa ajili ya kusapoti huduma.
Mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Kanda ya Ziwa Dede Petro
Share it:

matukio

Post A Comment: