WAMILIKI WA MAKAPUNI YA ULINZI WAMETAKIWA KUAJILI WATU WENYE MAFUNZO YA MGAMBO HILI KUDHIBITI JANGA LA KUUWAWA KWA WALINZI WILAYANI GEITA.

Share it:

Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi wa kushoto ni  Mwenyekiti wa kanda ya ziwa wa TAMASCA Charles Chacha Wakiwa katika kikao na wamiliki wa makapuni ya ulinzi Wilayani Geita.
Wajumbe wakifatilia kikao kwa makini zaidi wakiwemo kamati ya ulinzi na usalama Wilayani hapo.



Meza kuu ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita.

Mkuu wa wilaya ya Geita ,Herman Kapufi akifatilia kwa makini maoni na ushauri uliokuwa ukitolewa na wakurugenzi wa makapuni ya ulinzi.


Mkurugenzi mtendaji wa umoja Geita SecurityJoseph Mditi  akielezea namna ambavyo wanafikilia wao kama wamiliki wa makapuni ya ulinzi wanaweza kutokomeza mauwaji ya walinzi ambayo yamekuwa yakiibuka mara kwa mara.


Mkuu wa polisi Wilaya ya Geita, Ally Kitumbo Akisisitiza namna ambavyo jeshi la polisi wilayani hapo lipo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makapuni ya ulinzi.

Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Geita ,Agwaro Kenedy amesisitiza swala la makapuni kutumia taratibu zinazotakiwa kuwapatia ajira kwa kutumia viongozi wa mitaa.

Kaimu afisa tawala Wilaya ya Geita,Janeth Mobe,akiwashauri wamiliki kudumisha upendo na ushirikiano.
GEITA:Wilaya ya Geita ni miongoni mwa Wilaya inayokabiliwa na mauwaji ya walinzi ya mara kwa mara hali ambayo imeendelea kutishia usalama wa baadhi ya wananchi wanaofanya kazi hizo za  ulinzi kuziogopa na mwishowe kujikuta wengi wanaacha kutokana na kuhofia maisha yao.

Kutokana na hali hiyo imemlazimu Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi kukutana na wamiliki wa makapuni  ya ulinzi yanayofanya kazi wilayani humo lengo likiwa ni kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili walinzi katika maeneo yao ya kazi.

Charles Mwita ambaye ni Makamu  mwenyekiti wa makapuni ya ulinzi amesema kwamba ni kipindi kirefu sasa walinzi wameendelea kuuwawa na kwamba swala la mshahara kuwa mdogo ni sababu ambayo haina mashiko kwani wanachodhani wao yawezekana kukawa na kikundi ambacho kinafanya mauwaji hayo.

Hata hivyo Kaimu katibu tawala wa wilaya Geita Janeth Mobe ameomba mashirika hayo  kuwa na upendo lakini pia amewashauri Wakurugenzi kujenga mauhusiano na watumishi waliwaajiri.

“Natambua kuwa upendo ni swala  muhimu sana katika shughuli zetu za kila siku ni vyema kwa makampuni ya ulinzi kuwa na upendo lakini pia ni muhimu kuwa karibu na wafanyakazi ambao mnawaajiri unakuta Mkurugenzi wengine hajawahi kukutana hata siku moja na wafanyakazi wake hali ambayo inapelekea kushindwa kujua shida za wale uliwaajiri”alisema Mobe

Aidha kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi amewaagiza wamiliki wa makampuni kuwa na walinzi ambao wanakuwa na afya njema lakini pia wawe wamepitia mafunzo ya mgambo, na pia ameagiza mikesha yoyote ya kidini pamoja na kumbi  za starehe kuhakikisha wanakuwa na vibali na wanafunga kwa wakati sahihi maeneo ambayo wanafanyia biashara na yale ambayo wamekuwa wakiendesha ibada ili kudhibiti uharifu ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara.


 Imeandaliwa na Joel Maduka.

Share it:

habari

Post A Comment: