MWANAFUNZI ABAKWA NA KISHA KUNYONGWA.

Share it:






Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli

Bukombe. Mganga Mkuu Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Dk Aubery Mushi amesema kifo cha mwanafunzi aliyekutwa nyumba ya kulala wageni Septemba 29, kimetokana na kubakwa na baadaye kunyongwa.

Akizungumza tukio hilo , Dk Mushi alisema uchunguzi umebaini kuwa kabla ya kunyongwa, mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma kidato cha nne Sekondari ya Katente, Zainab Salum (18), aliingiliwa kimwili na watu wawili, mmoja akitumia kondomu na mwingine hakutumia.

Alisema uchunguzi unaonyesha mtu mmoja alimshika miguu na mwingine kumnyonga shingo kwa kutumia mikono baada ya kumbaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema wanamshikilia mwalimu mmoja wa sekondari, anayedaiwa kuwa na uhusiano wa mapenzi na mwanafunzi huyo.


Share it:

matukio

Post A Comment: