Mwenyekiti wa chama cha waanishi wa habari(GPC)Mkoani Geita Daniel Limbe akitoa tamko na kulaani vikali juu ya tukio walilofanyiwa waandishi wa habari. |
Waandishi wa habari wakimfatilia kwa makini mwenyekiti wa GPC |
Viongozi wa GPC wakiwa kwenye kikao cha waandishi wa habari kulia ni Victor Bariety ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama hicho na kushoto ni katibu wa GPC Salum Maige . |
Chama cha
waandishi wa habari Mkoani Geita(GPC) kimelaani vikali kitendo cha kushambuliwa kwa waandishi habari na jeshi la polisi wakati wakiwa katika majukumu yao ya kikazi.
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema leo ,mwenyekiti wa chama hicho Mkoani humo,Daniel
Limbe,amesema kuwa swala lililofanyika kwa kushambuliwa kwa waandishi wa habari
ni mwendelezo wa jeshi hilo kuminya
uhuru wa habari kwa watanzania ambao walipenda kujua ni kipi ambacho kilijiri
siku ya jana.
“Kama chama
cha waandishi Mkoani Geita,tumesikitishwa sana na kitendo cha jeshi polisi
kuwavamia waandishi na kuwapiga sisi kama chama tumeona hatuwezi kukaa kimya
swala hili tunalilaani vikali kwani ni mwendelezo wa uonevu kwa waandishi wa
habari hapa nchini kupitia kwa jeshi la polisi”Alisema Limbe
Hata hivyo Limbe
amemtaka Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba kujitokeza hadharani na kutoa tamko juu ya
tukio lililofanywa na askali ambao wamehusika na kitendo cha kuwapiga waandishi
wa habari .
“Sisi kama
chama cha waandishi wa habari mkoa wa Geita tunamwomba sasa Waziri wa Mambo ya ndani , Mh Mwigulu
Nchemba kujitokeza hadharani na kutoa
tamko dhidi ya jeshi la Polisi kutokana na unyanyasaji wanaofanya kwa
wanahabari na vyombo vya habari kimsingi tunaomba asimame na kuwaeleza wa
watanzania kuhusiana na tukio la jana kama vitendo vilivyo fanywa na jeshi la Polisi kama ni yake
au maagizo ya mkuu wa polisi wa mkoani Geita ama ni ukiukwaji wa taratibu za kiutumishi wa
vijana wa jeshi la polisi”Alisisitiza Limbe
Aidha baadhi
ya wananchi Mkoani humo wamelaani kitendo walichofanyiwa waandishi wa habari
kuwa swala hilo ni ukiukwaji wa sheria za nchi na kutokutoa uhuru vyombo vya
habari kuripoti vitu ambavyo vinakuwa vimejitokeza.
Hali hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tangu kutokea kwa
tukio hilo wakati waandishi wa habari wa
storm fm na channel ten walipokuwa
wakifatilia taarifa ya kukamatwa kwa waziri mkuu mstaafu wa awamu ya nne na
mjumbe wa kamati kuu wa Taifa
chadema,Edward Lowasa kukamatwa akiwa anatokea Mkoani Kagera wakati alipokuwa
akisalimiana na wananchi kwenye eneo la stend ya zamani.
IMEANDALIWA NA ,MADUKAONLINE
Post A Comment: