Mganga mkuu wa wilaya ya Geita Raphael Mhina ,akiwaeleza wananchi hali ya dawa ilivyo kwasasa katika wilaya ya Geita. |
Wananchi wa kata ya Katoro wakifatilia kwa makini kile ambacho kilikuwa kikijili katika Mkutano huo. |
Wananchi wa
mamlaka ya mji Mdogo wa Katoro Mkoani Geita, wamekubali utendaji wa kazi
alioanza nao Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Heriman Kapufi wa kuzunguka na
kuzungumza na wananchi kusikiliza kero zao na kuzitatua swala ambalo ni kinyume na viongozi baadhi
ambao wamepita hapo nyuma.
Wakizungumza katika
Mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Katoro wananchi hao walisema kuwa
Mkuu huyo wa wilaya ameletwa na mwenyezi Mungu hivyo wanaimani naye kuwa
atakuwa mstari wa mbele kutatua kero zinazowakabili.
Katika
Mkutano huo wananchi walitoa changamoto mbalimbali, huku sekta ya afya
ikilalamikiwa na wananchi wengi ambapo akina mama walisema wamekuwa hawapatiwi
huduma inayotakiwa.
“Mkuu wetu
wa wilaya tukueleze tu, sisi hatuna mashaka na wewe kwa jinsi ulivyo umekuwa na
hofu ya Mungu tunajua maendeleo kwa wilaya yako ya Geita yatakwenda kwa kasi viongozi
wengi hapa Geita wamekuwa wakitusimamia na kututofautisha kutokana na hali zetu za kimaisha mambo yaliyokuwa
yakikwamisha kutokana na migongano watu
wa Katoro tulikuwa wachangiaji wakubwa katika maendeleo ya kata yetu,’’ alisema
mkazi wa katoro
DC Kapufi
ambaye amekuwa akimtanguliza Mungu katika vikao vyake na mikutano mbalimbali ya wananchi, huku akiuhubiri
upendo kwa wananchi jambo ambalo limewavutia wengi huku wakiahidi kumpa
ushirikiano ili kuijenga Katoro na Geita kwa ujumla ambayo imetawaliwa na
itikadi za kisiasa huku miradi
mbalimbali ya maendeleo ikikwamishwa na baadhi ya wanasiasa.
Post A Comment: