Baadhi ya waandishi
wa habari wakiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu wa Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano wa Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) mara baada ya Taasisi
hiyo kutiliana saini makubaliano ya
Serikali imepanga kutumia bilioni 15 kuwapatia vijana stadi za kazi
zitakazowawezesha kujiajiri na kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa Viwanda.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam wakati wa kutiliana saini
makubaliano ya ushirikiano kati ya Taasisi ya Teknolojia Dar es saalam (DIT) na
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
Akizungumzia makubaliano hayo Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya
Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Ally Msaki amesema kuwa
yatasaidia kuiwezesha Taasisi hiyo kutoa mafunzo kwa vijana hasa ya kuzalisha
bidhaa zitokanazo na ngozi ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa
viwanda.
“Vijana 1000 wataanza kupata mafunzo mwezi Februari mwaka huu na
yatakayohusu utengenezaji wa bidhaa za ngozi na program hii ipo ndani ya mpango
wa miaka mitano.” Alisema Msaki.
Mafunzo hayo ya stadi za kazi kwa vijana yatagharimiwa na Serikali na
yatahusisha vijana walio katika mfumo rasmi na wale wasio katika mfumo rasmi wa
elimu lengo likiwa ni kuwakwamua vijana ili washiriki kikamilifu katika ujenzi
wa taifa.
Akifafanua Msaki alisema kuwa dhamira ya Serikali ni kuwawezesha vijana
baada ya mafunzo hayo kujiajiri na kuwaajiri wenzao hivyo kuondokana na tatizo
la ajira na kuongeza nguvukazi ya taifa kwenye uzalishaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT)
Prof.Preksedis Ndomba alibainisha kuwa Taasisi hiyo imejipanga vyema
kuwawezesha vijana kwa kutoa mafunzo yanayoendana na mahitaji ya soko na kuweka
msisitizo katika mafunzo kwa vitendo.
Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) ipo imedhamiria kutekeleza kwa
vitendo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda na
kufikia uchumi wa kati.
Imeandaliwa na Fatma Salum-MAELEZO
|
Post A Comment: