Wahanga 15 wakiwemo watanzania 14 na raia mmoja wa
kichina walionusurika na kifo baada ya kuokolewa kutoka chini ya ardhi
kwenye mgodi wa dhahabu wa RZ union
ulioko kijiji cha mawemeru kata ya Nyarugusu mkoani Geita baada ya kukaa
siku 3 bila chakula wala huduma yoyote wameruhusiwa kutoka Hospital ya mkoa wa
Geita walikopelekwa kupata matibabu.
Akiwaaga
baada ya kuruhusiwa kutoka hospitari Mkuu wa Mkoa wa huo,Meja Jenerali Mstaafu
Ezekiel Kyunga,amewaomba kurudi na kuendelea kujituma katika shughuli ambazo
wanafanya ili kuendelea na ujenzi wa
Taifa.
“Mko imara
sasa mrudi mkaendelee tena na ujenzi wa Taifa letu shughuli hizi ndio
zitawasaidia kupata kipato tumefarijka sana miongoni mwenu hayupo hata mmoja
aliyeteteleka”Alisema Kyunga.
Hata hivyo
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi,amesema kuwa wamekubaliana na mgodi
huo wafanyakazi wote katika mgodi huo kupatiwa mkataba ambao utawasaidia
wafanyakazi na pia amewaomba kuwa na mahusiano baina ya wafanyakazi na Waajili
ambo ni Raia wa china na pia amewasisitiza kumrudia Mungu kwani amewanusuru na
kifo.
Aidha kwa
upande wake Mwanasheria wa mgodi huo,Francis Kiganga pamoja na kuwashuru
mashirika ambayo yamejitolea kufanya shughuli za uokoaji pia amemwakikishia
mkuu wa wilaya kuongeza mkataba wa kazi badala ya miezi mitatu hatawapa wa
mwaka mzima.
Akiwaruhusu
wahanga hao, mganga mfawidhi wa Hospital ya mkoa wa Geita Dk. Brian Mawalla
amesema wamefikia uamuzi wa kuwaruhusu baada ya kujiridhisha na maendeleo
mazuri ya afya zao.
Wahanga hao
Wameokolewa January 29 mwaka huu kwa msaada kutoka makampuni ya Busolwa
Mining,Nyarugusu,GGM na ACACIA wamefanikiwa kuwaokoa watu hao waliofukiwa na
udongo wa kifusi cha mgodi huo Januari 26 mwaka huu.
Post A Comment: