CCM KIMENUKA MASHABIKI WA LOWASSA WATUPIWA VIRAGO ARUSHA

Share it:



CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha inadaiwa kimewafukuza uanachama baadhi ya vigogo wake akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Arusha, Wilfred Soileli.

Wanachama hao wanatuhumiwa kukisaliti chama hicho kabla na baada ya uchaguzi mkuu wakidaiwa kuwa wafuasi watiifu kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Wengine waliotimuliwa ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa kutoka jimbo la Arumeru Magharibi Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC ) na mfanyabiashara maarufu wa madini ya vito, Mathias Manga na Julius Mungure wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

Wakati vigogo hao mkoani Arusha ikielezwa wamevuliwa uanachama wiki iliyopita, Kamati ndogo ya Maadili ya CCM iliyokutana Dodoma iliwahoji wanachama wake ambao wanadaiwa kukisaliti chama hicho.

Hao ni Profesa Juma Kapuya, Nazir Karamagi na Ally Sumaye ambao wote wanadaiwa kukisaliti chama wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Wana CCM hao waliohojiwa na kamati hiyo iliyoongozwa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Rodrick Mpogolo, ambaye gazeti hili lilipomtafuta kwa simu, haikupokewa.

Taarifa zilizosambaa jijini hapa jana jioni zilidai uamuzi wa kuwafukuza uanachama viongozi hao ulifanyika katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Arusha kilichofanyika Jumamosi chini ya Mwenyekiti wa chama wa mkoa huo, Lekule Laizer.

Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho walisema kuwa Soileli na Manga walituhumiwa kushirikiana kutoa siri na mikakati ya chama na kuipeleka kwa viongozi wa Ukawa hasa Lowassa ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ya Rais.

“Hawa walionywa mara nyingi waache tabia ya kushirikiana na wapinzani hasa Lowassa lakini Manga aliwahi kusema yuko tayari kuchukuliwa hatua lakini asingeacha urafiki wake na Lowassa kwani siasa siyo uadui,” alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho ambaye hakutata kutwa jina .
Share it:

habari

Post A Comment: