MKUU WA WILAYA AKATAZA WANANCHI KUTUMIA MBUZI KATORIKI SABABU HIZI HAPA

Share it:
Image result for NGURUWE

Walaji wa nyama ya nguruwe ‘kitimoto’ wilayani Kalambo mkoani Rukwa watakikosa kitoweo hicho kwa muda usiojulikana baada ya Serikali kupiga marufuku watu kula nyama hiyo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya nguruwe 150 kufa kwa ugonjwa wa mafua wa African Swine Fever na kuwaacha wengine wakiwa hoi.

 Mkuu wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Julieth Binyura alisema ugonjwa huo ulijitokeza miezi mitatu  iliyopita kwenye Kitongoji cha Masazi  na kusambaa  katika kata za Legezamwendo  na Mambwe Nkoswe.

Ofisa Mifugo wa Wilaya ya Kalambo, Wilbroad Kansapa  alisema nguruwe wote wanaozagaa mitaani watakamatwa na mizoga yote ifukiwe.
Share it:

matukio

Post A Comment: