|
Wakili wa serikali Mkoani Geita,Emily Kiria akielezea namna ambavyo jamii ya wanasheria wanavyoweza kutoa haki na usawa kwa uhalisia na kwa wakati usika. |
|
Baadhi ya mawakili wa serikali na wananchi wakiwa wanasikiliza na kufatilia kilichokuwa kikiendelea. |
|
Wananchi wakisikiliza na kufatilia tukio lilivyokuwa likiendelea. |
|
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakitoa burudani kwenye maadhimisho hayo Mkoani Geita. |
|
wakili kutoka chama cha mawakili Tanzania(Tanganyika
law society),Bernad Otieno.akieleza namna ambavyo mahakama inatakiwa kutoa haki kwa wananchi. |
|
Kaimu hakimu Mfawidhi wa Mkoa wa Geita,Kariho Mrisho,,akiendelea kutoa maelezo namna mahakama ilivyojipanga kuendelea kutoa haki. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ,Meja
jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,akisisitiza swala la maadili kwa watumishi wa mahakama Mkoani Humo. |
|
Lothan Simkoko akitoa neno la shukrani kwa watu ambao wamejitokeza kwenye maadhimisho hayo. |
|
Baadhi ya mawakili wakiwa kwenye picha ya pamoja. |
Jamii ya
wanasheria Mkoani Geita imetakiwa kutoa
haki kwa misingi na sheria ikiwa ni pamoja na kuzingatia swala la muda kwenye
kesi ambazo wanazisimamia.
Kauli hiyo
imesemwa na wakili wa serikali Mkoani humo Emily Kiria wakati wa maadhimisho ya wiki ya
sheria,ambapo ameeleza kuwa jamii ya wanasheria
wote wawe wa serikali na wakujitegemea wanajukumu la kuhakikisha wanatoa
haki kwa uharisia na ukweli kwa swala usika.
“Jamii ya wanasheria na hili ni jukumu la
wanasheria wote wawe wa serikali au wa kujitegemea wanalo jukumu la kuhakikisha
wanatoa haki kwa uharisia na kwa ukweli wa swala usika na siyo kuhakikisha tu
kwamba wanawatetea au kuwasaidia watu kwasababu tu wamefika kuomba msaada”alisema
Kiria
Kwa upande
wake wakili kutoka chama cha mawakili Tanzania(Tanganyika law society),Bernad
Otieno,alifafanua kuwa mahakama
inawajibu wa kusikiliza malalamiko yanayoletwa na wananchi na kuyatolea
mahamuzi wajibu huo ni wa kikatiba kwani inatokana na jamhuri ya mwaka 1977
kama ilivyofanyiwa marekebisho katiba ibara ya 107 (A) ibara ndogo ya kwanza na
ya pili.
Mkuu wa Mkoa
wa Geita ambaye alikuwa mgeni rasmi
kwenye maadhimisho hayo ,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,ameendelea
kusisitiza swala la muda wa kusikiliza kesi ,pamoja na kuwataka watumishi wa mahakama kuwa wahadilifu na waaminifu kwenye shughuli
zao.
“Naomba
kutoa wito kwa watumishi kuendesha kesi kwa muda usika ikiwa ni pamoja na kuwa
waaminifu katika shughuli zenu za kila siku za kutoa haki kwa wananchi”alisisitiza
Kyunga
Siku ya Sheria
nchini ilioanzishwa mwaka 1996 ikiwa ni siku muhimu ya kuombea Majaji na
Mahakimu ili kuweza kusikiliza kesi
ambapo kitaifa imefanyikia jijini Dar es salaam na Mgeni Rasmi akiwa ni Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt. John Pombe Magufuli,kauli mbiu
ikiwa ni Utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: