: NAPE: NITAHAKIKISHA TIMU ZA DODOMA ZINACHEZA LIGI KUU.

Share it:

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na vijana wa Jogging club Mjini Dodoma mara baada ya kufanya mazoezi ya pamoja yenye nia ya kuimarisha afya na kuendeleza michezo nchini yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma leo March 1, 2017. 


Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewahakikishia wapenzi wa Mpira Mjini Dodoma kuwa timu za Mpira Mkoani humo zitashiriki Ligi Kuu ili kuwapa raha ya Ligi hiyo mashabiki wa mpira na michezo kwa ujumla.

Amezungumza hayo mara baada ya kukutana na kufanya mazoezi na Vijana kutoka Jogging Club mbalimbali Mjini Dodoma ikiwa ni ishara rasmi ya Wizara yake kuhamia katika Makao Makuu ya nchi.

Mhe. Nape Nnauye amesema kuwa haitawezekana Serikali ikahamia Dodoma na kusiwe na timu inayoshiriki Ligi kuu ya Mpira wa Miguu Tanzania Bara hivyo yeye kama Waziri anayehusika na Michezo kwa kushirikiana na wadau wa Michezo atahakikisha Timu zinafanya vizuri na kushiriki Ligi hiyo.

“Haiwezekani Rais akawa hapa na Makamu wa Rais na Mawaziri tukakosa ladha na furaha ya Ligi kuu hapa Dodoma nitahakikisha timu za hapa zinashiriki Ligi kuu”alisistiza Mhe. Nnauye.

Kwa upande wake  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde amewapongeza vijana wa Jogging club na wakazi wa Dodoma kwa kushiriki michezo na kuhimiza kujituma zaidi kwa timu za michezo hasa mpira wa miguu ili kushiriki Ligi kuu Tanzania Bara.

Naye Katibu Mkuu Wizara wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewaomba wakazi wa Dodoma kufanya michezo kuwa ni Utamaduni wao wa kila siku ili kujenga Taifa la wapenda michezo kwa nia ya kuimarisha afya na kuendeleza michezo nchini.

Aidha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Nchini Bw. Omary Singo amewahakikishia wakazi na wapenzi wa Michezo ushirikiano katika kuendeleza na kukuza michezo hasa katika makao makuu ya nchi Dodoma.
Share it:

michezo

Post A Comment: