Shukurani za pekee pia ziwaendelee best man na best lady, Mr and Mrs, Joel Maduka kutoka Storm Fm Geita na Maduka Online kwa kufanikisha shughuli hiyo kwenda vyema.
Maduka online inakusihi uendelee kutazama picha za awali za shughuli hiyo wakati wataalamu wetu wakiendelea kukuandalia picha nyingine ikiwemo picha za kanisani.
Siku jumapili March 26,2017 ilikuwa siku muhimu kwa mwanahabari wa 102.5 Lake Fm Mwanza na mwanabloga wa BMG, George Binagi wa Tarime Mara pamoja na Miss Upendo Kisaka wa Moshi Kilimanjaro baada ya kuuaga ukapela.
Wapendanao hao walifunga pingu za maisha katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza na baadaye hafla kufanyika Ukumbi wa Sun City Hotel, Ghana Green View Jijini Mwanza.
Akizungumza na Maduka Online Amewashukuru wote ambao wameshiriki kufanikisha Shughuli Hiyo.
"Ahsanteni nyote mliotusaidia kutimiza ndoto yetu kubwa katika maishani yetu. Familia yangu, ndugu, jamaa na marafiki zangu. Waumini wote wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Daniel Kulola na kila mmoja kwa nafasi yake, Mungu awabariki. Mmenionesha upendo wa ajabu mno.
Wazazi wangu hususani mama mpendwa, nimetimiza deni mliloniachia duniani, hakika sasa mtapumzika kwa amani, pahali pema, peponi, Amina. Ndoa na iheshimiwe na watu wote, Mungu atuongoze vyema". Mr & Mrs George Binagi.
Maduka Online Inachukua Fursa Hii hadhimu kuwapongeza sana Bw na Bi George Binagi kwa hatua hii na pia upendo na amani vitawale siku zote kwenye maisha yenu ya Ndoa Kubwa zaidi Mkimtanguliza Mungu.



























Post A Comment: