WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA MPANGO WA USAJILI NA UTOAJI WA VYETI VYA KUZALIWA KWENYE MIKOA YA GEITA NA SHINYANGA

Share it:
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt Harrison Mwakyembe(MB) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa Mkoa wa Geita na Shinyanga,wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga na Wakwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainabu Telack wengine ni wawakilishi wa Mashirika ya Maendeleo ya kimataifa pamoja na viongozi Mbalimbali wa Dini na vyama vya Siasa.

Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe akionesha simu janja ambayo itatumika kwenye zoezi hilo.








Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe  amezindua Mpango wa Usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri wa miaka  Mitano kwenye mikoa ya Geita na Shinyanga.

Uzinduzi huo ambao umefanyika kwenye viwanja vya kalangalala mjini Geita,umehudhuriwa na wakuu wa Mikoa yote Miwli  pamoja na viongozi wa wakuu wakiwemo wakuu wa wilaya,wakurugenzi watendaji wa halmashauri zote,makatibu tawala wa mikoa na wilaya,waganga wakuu wa mikoa hiyo,waganga wakuu wengine wa idara na wananchi mjini Hapa.

Akito Takwimu za sense ya watu na makazi ya mwaka 2012  Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya wakala wa usajili,ufilisi na udhamini(RITA) Bi,Victoria Lembeli,amesema kuwa  ni asilimia kumi na tatu pointi nne ya wananchi wa Tanzania Bara ndio ambao wamesajiliwa na kupatiwa vyeti hali ambayo sio nzuri kwa Taifa.

Kwa upande wa UNICEF, Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Tanzania Rene Van Dongen alisema “ Kila mtoto ana haki ya kutambuliwa  na Cheti cha kuzaliwa ni taarifa muhimu ya awali inayothibitisha kuzaliwa kwa mtoto,Kwa sasa Tanzania ina kiwango cha chini sana cha usajili wa watoto, hali inayoashiria idadi kubwa ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano hawatambuliki katika taarifa za serikali , Mpango huu utaongeza kasi ya usajili wa watoto na fursa ya kupata haki yao ya msingi na kwa upande wa serikali itakuwa na taarifa sahihi kwa ajili ya mipango na sera”Alisema Dongen.

Serikali ya kanada ambayo ni mfadhili wa mpango huu inatambua haki za watoto na ina amini kila mtoto anahitaji utambulisho wa kudumu wa kuzaliwa unaotambulika na nchi kisheria na ni haki ya msingi ya mtoto.  Ufadhili umechangia juhudi za serikaliza kuboresha mpango wa kuduma wavyeti vya kuzaliwa unaoenga kufikia watoto million tatu na nusu (3.5 million) walio.


Kampuni ya simu za mikononi TIGO ni mshiriki wa mpango huu kwa kutoa ufadhili wa Tehema, ambao umerahisisha taarifa za usajili kuingizwa kwenye mfumo wa Takwimu wa RITA moja kwa moja. TIGO imechangia uhamasishaji wa umuhimu wa usajili katika jamii.

Meneja wa Kanda ya Ziwa wa TIGO Ally Maswanya, alisema kuwa Ushiriki wa TIGO uko katika mpango wa kuboresha matumizi ya digital katika maisha kwa kushirikiana na UNICEF na RITA kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa anapata fursa ya kuandikishwa na kwamba kuna wanafurahia  kuona matokeo ya mpango huu toka uanze mwaka 2013 umebadili taswira ya huduma ya usajili wa watoto. 

Kampuni ya TIGO imechangia  simu za za mkononi elfu moja na mia mbili (1,200) zenye gharama ya shilingi  Milioni 113  kuwawezesha waratibu wanaotekeleza usajili katika mikoa ya Geita na Shinyanga  kufanya kazi yao kwa ufanisi “ alisema Maswanya.


Akiwahutubia wananchi mgeni rasimi kwenye uzinduzi huo ambaye ni  Waziri wa katiba na sheria Dkt,Harrison Mwakyembe,amewaasa watanzania Kujenga utamaduni wa kusajili kila mtoto anayezaliwa ili aweze kutambuliwa ndani na muda mfupi baada ya kuzaliwa kwake ikiwa ni pamoja  na kutoa taarifa za kila mtu anayefariki .

Baadhi ya wananchi ambao wamezungumza na Maduka online  Mkoani Humo, Ivon Mashaka  na Abubakari Magembe wamesema kuwa wanaishukuru serikali kwani imerahisisha kwa wananchi wasiyokuwa na uwezo kupata vyeti bila ya gharama yoyote.


Mpango wa usajili wa  wa vizazi na vifo utasaidia kuziba pengo la mgawanyo uliopo kati ya mijini na vijijini kwa kupeleka huduma za usajili kwa watoto walio chini ya umri wa Miaka mitano kwa jamii zilizoko pembezoni.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE



Share it:

habari

Post A Comment: