KANISA LA AICT LAWATUMBUA VIGOGO WATANO MKOANI SHINYANGA,YUMO ASKOFU NKOLA NA KATIBU MKUU JAKOBO MAPAMBANO.

Share it:

Kanisa la AICT nchini Tanzania limemstaafisha askofu mkuu wa kanisa hilo Dkt John Kanoni Nkola na kumtaka askofu mwingine wakanisa hilo John Bunango kujiuzula nafasi hiyo kutokana na matumizi mabaya ya fedha za kanisa.

Kanisa hilo pia limefukuza kazi ya uchungaji wachungaji watatu ambao ni Katibu mkuu wa kanisa hilo Mchungaji Jakobo Mapambano,mchungaji Dkt Meshack Kulwa.
na Mchungaji Emmanuel Isaya.

Hatua hiyo imechukuliwa siku chache tu baada ya Shule inayomilikiwa na kanisa hilo kupigwa mnada na kulisababishia kanisa hilo hasara.


Tangazo la kanisa kuchukua hatua hizo limetangazwa muda huu katika kanisa la AICT Kambarage na Askofu mkuu wa kanisa la AICT nchini Tanzania Askofu Silasi Kezakubi (pichani) kutokana na maamuzi ya baraza la utendaji la sinodi kuu AICT.

CHANZO NI MALUNDE 1 BLOG.
Share it:

habari

Post A Comment: