CCM YAMPA MAKAVU LOWASSA

Share it:
Image result for LOWASA

Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha kimeishangaa kauli ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kusema kuwa Rais John Magufuli amemtuma ‘mtoto mdogo’ kwenda kuiwakilisha serikali kwenye mazishi ya wanafunzi wa  shule ya Lucky Vicent

 Akizungumza  na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Michael Lekule ,alisema kauli ya Waziri huyo mstaafu ameitoa kwa kudanganya wananchi na kuonesha serikali ya Magufuli haishirikiani na wananchi ,wakati serikali iliubeba msiba huo mzito wa taifa.

 Alisema jitihada za serikali ya Magufuli zimeonekana kupitia kwa wawakilishi wake Makamu wa Rais Samia Suluhu pamoja na Mrisho Gambo pamoja na wanachama wa CCM ambao walijitokeza kwa wingi kwenye msiba huo mzito

 "Serikali ilijitoa kwa hali na mali kuwezesha  familia 35 kwenda kupumzisha wapendwa wao,na ilihakikisha kila mwili unapumzika mahala popote familia inapopata,tunajiuliza walitaka nini kama kote nafasi ilijazwa na serikali ya Magufuli," alisema Michael

 "CCM inakanusha kwanguvu upotoshaji huo,hata ukiangalia siku ile uwanja wa shekh Amri Abeid wanaccm walijaa uwanjani ,kikubwa CCM imeguswa na msiba uliotokea na Rais wetu amekuwa bega kwa bega juu ya tukio lililotokea,"alisema

 Pia alisema wamemshangaa kwa kusema Rais alimtuma mtoto mdogo wakati yeye mwaka 2007 ajali mbaya iliyotokea Monduli duka bovu na kuua watu 20 ambao 11 walikuwa ni askari wa JKT,rais Kikwete alimtuma aje kuiwakilisha serikali.

 Hata hivyo alimtaka kiongozi huyo, ajiulize kama yeye kipindi akiwa Waziri Mkuu aliweza kutumwa na Rais, amuwakilishe kwenye msiba wa watu 20, je yeye na Makamu wa Rais ni nani mdogo?

 "Tena ajali hiyo ilikuwa ya kitaifa,askari 11 walifariki kwenye ajali,mbona hajayasema ya kwake?," alisema Lekule
Share it:

SIASA

Post A Comment: