Bwawa la Maji la Kunyweshea mifugo likiwa kwenye eneo ambalo ni karibu na sehemu ya Kiwanda cha kuchenjulia Dhahabu.
Wananchi wa
Kijiji cha Hililika Kata ya Nyarugusu Wilaya na Mkoa wa Geita wameandamana kupinga mwekezaji kuweka kiwanda
cha kuchenjulia Dhahabu kwa madai kuwa chanzo cha maji ambacho wanakitegemea
kijijini hapo kipo karibu na planti ambayo inajengwa na kwamba inaweza kusababisha
madhara ya afya kutokana na Kemikali yaCyanide ambayo hutumika kwenye shughuli za uchenjuaji.
Wakizungumza
na mtandao wa maduka online kwa vipindi Tofauti wamesema kuwa hofu kubwa waliyonayo
ni kutokana na sumu ya kuchenjulia
dhahabu kwani ni hatari kwa afya zao na viumbe ambavyo vinazunguka maeneo
ambayo wanafanyia kazi.
“Sehemu hii
ni karibu sana na eneo ambalo tunachotea maji sasa kama wakiweka hicho kiwanda
sisi wananchi tutakuwa kwenye hali gani hebu serikali ijaribu kulitazama swala
hili kwa umakini zaidi tutaisha kutokana na sumu ya kuozesha marudio”Alisema
Bi,Hellen Mbaru.
“Sawa eneo
hili ni la mtu Binafisi na lipo ndani ya kijiji cha Hililika na kwamba
tunaambiwa kuwa watawapa angalizo wawekezaji ndani ya mwaka mmoja endapo kama
kuna maafa ambayo yatajitokeza watawafukuza kweli na hali hii jamani hadi watu
wadhurike ndio tahadhili ichukuliwe mimi naomba sana serikali ilitazame hili”Alisema
Hata hivyo
Lawama nyingi zimemwangukia Mwenyekiti wa Kijiji kuwa amehusika kwa kiasi
kikubwa Kwa kuchukua rushwa kutoka kwa mwekezaji na kwamba kwa sasa hawana
imani naye hali ambayo imesababisha kufunga ofisi ya Kijiji.
Kutokana na
hali hii askari Polisi wamefika kwenye eneo hilo na kumshauri Mwenyekiti wa
Kijiji hicho ambaye alifika kwenye eneo hilo kuona umuhimu wa kuwasikiliza
wananchi na kusitisha ujenzi wa Planti hiyo.
Hata hivyo
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Daniel Mwigulu Nkela,amesema kuwa maamuzi ambayo
yalichukuliwa hayakuwa ya peke yake bali ni ya wajumbe wote ambao waliridhia
eneo hilo.
“Maana ya
serikali kuna wajumbe 25 mimi kama mwenyekiti sina mamlaka ya kuidhinisha eneo
hili peke yangu mwekezaji anapotaka kuingia tunaitisha serikali ya kijiji
inakaa na inapokaa kuna kuwa na mahojiano kati ya mwekezaji na wajumbe wa serikali ya kijiji mimi kazi yangu ni kulinda
maadhimio kikao tu sina mamlaka ya kuhidhinisha eneo lolote lile”Alisema
Mwigulu.
Maduka
online imemtafuta mwekezaji wa eneo hilo kutaka kujua makubaliano yake na
serikali ya kijiji ambapo moja kati ya wasimamizi wa eneo wamegoma kuzungumzia swala hilo na kwamba
anaye weza kuzungumzia swala hilo ni meneja wao ambaye yupo Mwanza kwa sasa
hata hivyo jitihada bado zinaendelea kujua makubaliano yalikuwaje.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
|
Post A Comment: