KOREA KASKANI YAFANYA JARIBIO LINGINE LA KOMBORA AMBALO LILIPAA KILOMITA 500

Share it:



Korea Kaskazini imesema  kuwa ilifanikiwa kurusha kombora la masafa ya wastani siku ya jana  Jumapili.

Shirika la habari la taifa nchini humo KCNA lilisema kuwa zana hiyo sasa iko tayari kutumiwa kwa shughuli za kijeshi.

Ikulu ya White House ilisema kuwa kombora hilo lilikuwa la masafa marefu kuliko makombora yaliyotumiwa na Korea Kaskazini wakati wa majaribio matatu ya awali.

Jaribio hilo linakuja wiki moja baada ya Korea Kaskazini kufanyia jaribio la kile ilichokitaja kuwa kombora jipya lenye uwezo wa kubeba silaha za nuklia.

Jumatatu iliyopita baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilisema kuwa Korea haistahili kufanya majaribio zaidi.

Sasa baraza hilo linatarajiwa kukutana kwa faragha siku ya Jumanne kwenye mkutano ulioitishwa na Marekani, Korea Kusini na Japan.
 
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Korea Kusini imelitaja jaribio hilo kuwa la kiholela huku waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani akilitaja kuwa la kughadhabisha.

Kombora hio lilisafiri umbali wa kilomita 560 kuelekea bahari ya Japan. Kombora la wiki iliyopita lilisafri umbali wa kilomita 700.
Share it:

KIMATAIFA

Post A Comment: