NHIF YAZINDUA MPANGO WA MADAKTARI BINGWA GEITA

Share it:


Kaimu Mkurugenzi wa tiba na ushauri wa kiufundi NHIF Makao makuu ,Dr Aifena Mramba akielezea malengo ya kuwepo kwa madkatari Bingwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita wakati wa hafra fupi ya uzinduzi ambayo imefanyika kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo. 
Meneja wa NHIF Mkoani Geita Mathias Sweya Akitoa utambulisho mbele ya mgeni Rasmi wakati wa Hafra fupi ya uzinduzi wa Mpango wa Madaktari Bingwa.
Mgeni Rasmi Ambaye ni Katibu Tawala Mkoani Humo Celestine Gesimba  akizungumza na wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kwaajili ya huduma ya afya kwenye Hosptali ya Rufaa ya Mkoa.
Kaimu Mkurugenzi wa tiba na ushauri wa kiufundi NHIF Makao makuu ,Dr Aifena Mramba akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Celestine Gesimba Shuka mia moja ambazo wametoa kama msaada kwa hosptali hiyo.

Mzee Peter Fulano ambaye ametokea Chato kwaajili ya kuja kufanyiwa Huduma ya afya akishukuru kwa huduma hiyo kuwepo Mkoani humo uku akiomba huduma hiyo kufika pia kwenye Wilaya ambazo zipo ndani ya Mkoa.

Bi,Mariam Walwa ambaye ni Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Wilaya ya Geita akiomba kupatiwa nafasi na kipa umbele kwa wanawake kutokana na wao kuwa na majukumu mengi ya Kifamilia.

Meza Kuu ikifuatilia kile ambacho baadhi ya wananchi walikuwa wakikiomba.

Mgeni Rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa hospitali ya Rufaa na Madaktari Bingwa.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita  Brayn Mawala  akifafanua juu ya huduma ya afya kwenye Hospitali ya Mkoa.

Hodi ya wazee huduma zikiendelea.

Dr Mawala akimjulia hali moja kati ya wagonjwa ambao walikuwa kwenye hodi ya wazee.
Wananchi wakiwa kwenye Foleni wakisubilia huduma ya afya.

Nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.


Picha na Joel Maduka wa Maduka Online

Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya NHIF   umezindua mpango wa madaktari  Bingwa  Mkoani Geita  lengo likiwa ni kushirikiana na serikali kupunguza changamoto za upatikanaji wa huduma za kibingwa na kusogeza huduma karibu na wananchi pamoja na wanachama wa mfuko huo.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi wa tiba na ushauri wa kiufundi NHIF Makao makuu ,Dr Aifena Mramba amesema  watu elfu kumi na tatu mia moja na sitini na saba (13167) na kati ya hao mia nne sitini(460) wamekwisha kufanyiwa huduma ya upasuaji.

“Kabla ya kuleta madaktari bingwa kwenye Mkoa husika mfuko huwa unafanya tathimini na kubaini uhitaji katika kila Mkoa ndivyo hivyo tumefanya kwenye Mkoa huu wa Geita na kuamua kuleta madaktari bingwa kama ambavyo nimeeleza  kwa hiyo Tumekuja na madaktari Bingwa pamoja na Dawa na mashuka ambavyo vitasaidia kwenye huduma za kiafya”Alisema Mramba.

Aidha Bi, Mramba ameongezea kuwa matarajio ya mfuko huo ni kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali za ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na kutoa fursa kwa madaktari kutoa huduma kwa uhakika zaidi kwa watu wachache watakaolazimika kufuata huduma hizo kwenye hospitali Kubwa ikiwa ni pamoja na watumishi wa Hospitali husika kutumia fursa ya kujifunza kwa kupata ujunzi na utaalamu kupitia kwa madaktari wageni.

Kwa Upande Wake Mgeni Rasmi Ambaye ni Katibu Tawala Mkoani Humo Celestine Gesimba  amewata madaktari  kuwatumia madaktari bingwa waliofika Hospitalini hapo kutoa huduma kwa wagonjwa ili kujifunza mbinu mpya za utoaji wa huduma badala ya kwenda kufuata mbinu hizo nje ya maeneo yao ya kazi

Daktari Bingwa wa magonjwa ya Watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando Dr Neema Chami amesema tangu kuanza kwa huduma hizo kwa siku 2 sasa wamewahudumia watoto 80 hali inayoonesha mafanikio ya lengo la wao kufika mkoani humo.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita Dr Brian Mawala amesema ombi la Wananchi la kutaka Madaktari Bingwa wawe wanafika mara kwa mara Hospitalini hapo, litafanyiwa kazi kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF ili kupunguza wananchi wasisafiri umbali mrefu kufuata huduma za Kibingwa

Zoezi la utoaji wa huduma za upasuaji kutoka kwa Madaktari  Bingwa kwenye Mikoa ya  Geita na Kigoma  lilianza  rasmi Mei 22  siku ya jumatatu kwa uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF  ambapo hadi sasa ni jumla  ya wagonjwa 1,204 wamekwisha hudumiwa kwa siku mbili huku wagonjwa ambao wamefanyiwa upasuaji kwa mikoa  miwili ni kumi na nne.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE



Share it:

habari

Post A Comment: