TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

Share it:
msangii-1




TAREHE  14.05.2017 MAJIRA YA SAA 02:00HRS USIKU KATIKA KISIWA CHA GANA KILICHOPO KIJIJI CHA KAMASI KATA YA ILANGALA WILAYA YA UKEREWE, MTU ANAYEFAHAMIKA KWA JINA LA MKAMA MGENGELE, MIAKA 36, MVUVI NA MKAZI WA GANA KISIWANI, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMFANYIA UKATILI MTU ANAYEDAIWA KUWA MPENZI WAKE AITWAYE ESTER LAZARO MIAKA 37, MHUDUMU WA NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO BACELONA NA MKAZI WA GANA KISIWANI, KWA KUMKATA NA KITU CHENYE NCHA KALI KWENYE KIGANJA CHA MKONO WAKE WA KUSHOTO HADI KIKAANGUKA CHINI KISHA AKAMKATA TENA KWENYE PAJA LA MGUU WA KULIA, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA BI ESTER LAZARO KWA MUDA MREFU, LAKINI HIVI KARIBUNI WALIKUWA KWENYE MGOGORO WA KIMAPENZI, INASEMEKANA KWAMBA TAREHE TAJWA HAPO JUU MTUHUMIWA ALIFIKA KWENYE NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO BACELONA AMBAPO MPENZI WAKE BI ESTER ANAFANYIA KAZI HUKU AKIWA AMELEWA POMBE NA KUANZA KURUSHIANA MANENO MAKALI. INADAIWA ILIPOFIKA MAJIRA TAJWA HAPO JUU MTUHUMIWA ALIMWENDEA BI ESTER LAZARO HUKU AKIWA HAFAHAMU KINACHOENDELEA NA KUMKATA KWA KUTUMIA KITU CHENYE NCHALI KWENYE KIGANJA CHA MKONO WAKE WA KUSHOTO HADI KIKAANGUKA CHINI KISHA AKAMKATA TENA KWENYE PAJA LA MGUU WA KULIA KISHA AKAONDOKA ENEO LA TUKIO.
WANANCHI WALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA JUU YA TAARIFA HIZO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA. MTUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA UKEREWE AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWAOMBA KUACHA TABIA YA KUJICHULIA SHERIA MKONONI KWANI MADHARA YAKE NI MAKUBWA LAKINI PIA NI KOSA LA JINAI. AIDHA ANAWAOMBA WANANDOA AU WATU WALIOKUWA KWENYE MAHUSIANO YA KIMAPENZI KWA MUDA MREFU WAKIWA KWENYE MIGOGORO WAENDE POLISI KIPO KITENGO CHA DAWATI  AMBACHO KINAWATAALAMU WANAOSHUGHULIKIA MATATIZO HAYO AU WAENDE KWENYE TAASISI NYINGINE ZA SERIKALI KAMA USTAWI WA JAMII NA SIO KUJICHULIA SHERIA MKONONI.
KATIKA TUKIO LA PILI;
MNAMO TAREHE  14.05.2017 MAJIRA YA SAA 18:30HRS JIONI KATIKA BARABARA YA MWANZA KWENDA SHINYANGA KIJIJI CHA NYANG’HOLONGO TARAFA YA USAGARA WILAYA YA MISUNGWI MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA T.571 BHU AINA YA MINBUS FUSO MALI YA MOHAMEDI MAMDALI LIKITOKEA MWANZA KWENDA KAHAMA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FREDY KAWASANGE  MIAKA 39, MKAZI WA KAHAMA, LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AITWAYE JUMA NKANU, ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA KATI YA 40 HADI 50, NA MKAZI WA KIJIJI CHA IBONGOYA “A” NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA ANAVUKA BARABARA BILA KUCHUKUA TAHADHARI YEYOTE  HUKU AKIWA AMELEWA NDIPO GHAFLA ALIKUTANA NA GARI TAJWA HAPO JUU LIKIWA KWENYE MWENDO KASI NA KUGONGWA NA KUPELEKEA MAREHEMU KUPOTEZA MAISHA.
DEREVA WA GARI HILO AMEKAMATWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHI HOSPITALI YA WILAYA YA MISUNGWI KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU PINDI WAWAPO BARABARANI AKIWATAKA KUWA MAKINI NA KUCHUKUA TAHADHARI WAKATI WOTE  ILI KUJIEPUSHA NA AJALI NA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA PIA ANAWATAKA WAENDESHAJI WA VYOMBO VYA MOTO KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARANI WAKATI WOTE ILI KUWEZA KUZUIA AJALI ZISIZO ZA LAZIMA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
Share it:

habari

Post A Comment: