WAKULIMA KUNUFAIKA NA BWAWA LA KILOMO CHA UMWAGILIAJI MKOANI GEITA

Share it:
Mkuu wa Wilaya ya Geita  Mwl Herman Kapufi akikagua Shamba la Mahindi kwenye Kijiji cha Nyang'uku .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Leornad Kiganga Bugomola akikagua Shamba la Uele kijiji cha Nyang'uku wakati wa ziara ya kutembelea wakulima Mashamba.
Mkuu wa Wilaya ya Geita na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita wakiwa kwenye Shughuli za kuangalia namna ambavyo wakulima wameitikia kulima kilimo ambacho kinastahimili ukame.




Diwani wa Kata ya Nyang'uko  Elias Ngole akiwatambulisha Viongozi ambao walikuwa wameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Geita.

Wana Kijiji wa Kijiji cha Nyang'uku wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Geita wakati alipokuwa akiwasisitiza kuendelea na shughuli za kilimo kwa kulima mazao ambayo yanastahimili ukame.

Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Mwl Herman Kapufi akizungumza na wanakijiji wa Nyang'uku.

Shamba la Mtama likiwa limestawi.

Mkuu wa Wilaya akiwa na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita pamoja na madiwani wakati wa kuzungukia mashamba Kwenye vijiji vya Nyang'uku,Ibanda na Bungwangoko.



Serikali ya Wilaya ya  Geita ,inatarajia kujenga mradi wa Bwawa la Maji   kwaajili ya Kilimo cha umwagiliaji kwenye vijiji vya  ibanda kata ya Kanyara Chabulongo na Mkoba kata ya  Bungwangoko ambapo utaghalimu jumla ya kiasi cha Sh,Bilioni mbili na nusu.

Akizungumza na Maduka online  ,Fundi Sanifu umwagiliaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Ally Semfukwe,amesema kuwa mradi ambao unatarajia kujengwa  utanufaisha vijiji vitano ambapo viwili vinatoka kwenye Halmashauri ya wilaya ya Sengerema na vingine vitatu kwenye wilaya ya Geita.

“Mradi huu wa Bwawa la maji naamini wakulima wataweza kufaidika nao kwani ni shughuli nyingi ambazo watakuwa wakizifanya tukiachana na Kilimo wanaweza kutumia pia kwaajili kunyweshea mifugo na kwamba kukamilika kwa mradi huo utaghalimu kiasi cha sh,Bilioni mbili na nusu”Alisema Semfukwe.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Modest Aporinali amebainisha  kuwa  eneo ambalo litatumika kwaajili ya shughuli za utengenezaji wa Bwawa hilo ni zaidi ya Hekari 500 hadi 1000 na kwamba maeneo hayo ni makazi ya watu na mradi huo ni wa serikali kuu ambapo wataangalia ni maeneo gani ambayo ni makazi ya watu kwaajili ya kuwalipa fidia wale ambao watakuwa wamefikiwa na mradi.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi amezungumza na wananchi wa kijiji chA Ibanda kata ya Kanyara wakati wa ziara yake ya kuzungukia kwenye kata ya Nyang’uku,Kasamwa ,Bungwangoko na Kanyara ambayo ilikuwa na lengo la kuangalia kilimo cha Mtama,Mhogo pamoja na pamba,wananchi hao mradio huo ukikamilika utaleta faida kwani awatakuwa wa kusubilia Msimu wa Mvua na kwamba maji yatapatikana muda wote pindi wanapoitaji kufanya shughuli za kilimo.

Hata hivyo pamoja na Mradi huo kuwa ni wamanufaa kwa wakulima ,baadhi ya wakulima wa kijiji cha Ibanda wamepinga Hatua hiyo na kusema kuwa wao wameshazoea kilimo cha zamani na kwamba yawezekana kisiwe na tija kwao kutokana na kwamba wanaweza wakajikuta wakilipia ghalama za kunyweshea mifugo yao.

Mradi wa umwagiliaji kama utakamilika unatarajia kuwanufaisha zaidi ya wananchi laki moja kutoka kwenye vijiji vitano.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE


Share it:

habari

Post A Comment: