Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki katika swala ya magaharibi katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu mjini Chato, mkoani Geita, Juni 21, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mussa Magwesera wa Kanisa la African Inland Church (AIC), Dayosisi ya Geita katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu kwa Niaba ya Rais John Pombe Magufuli mjini Chato mkoani Geita Juni 21, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifuturu pamoja na Askofu Mussa Magwesera wa Kanisa la African Inland Church (AIC) Dayosisi ya Geita (kushoto) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alhaj Yusuph Kabaju(kulia) katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli, mjini Chato, mkoani Geita Juni 21, 2017.
Serikali imewataka viongozi wa madhehebu
ya dini nchini kutumia majumba
yao ya ibada kuhubiri
amani badala kuhubiri
mahubiri yanayo weza kusababisha
mifarakano na jamii .
Kauli hiyo
imetolewa jana na
Waziri Mkuu wa
Kassimu Majaliwa wakati
akifuturu na waumuni
wa dini ya kislamu mjini
Chato mkoani Geita futari ambayo
imeandaliwa na Rais wa awamu ya tano
Dk, John Pombe Magufuli.
Alisema kuwa
viongozi wa madhehebu ya dini
hawana budi kuendelea kuhubiri amani na kuliombea Taifa wakati
wote ili kudumisha amani
na upendo ambao tumeachiwa na wa
waasisi wa Taifa hili
akiwemo Baba wa Taifa mwalimu
Julius Kambarage Nyerere badala ya kuibua
mifarakano ndani ya makanisa kama
kugombea madaraka .
Waziri mkuu
alisema kuwa serikali
ya awamu ya tano
inaheshimu na kuthamini mchango
wa madhehebu ya dini
katika kuliombea Taifa amani
na kwamba kila mmoja anayo haki ya kuabudu katika imani yake ya dini na hivyo kuwataka
viongozi hao kudumisha tunu ya amani ambayo
Mungu amewajalia watanzania .
Majaliwa ameongeza kuwa
madhehebu ya dini yana saidia
watoto kuwalea katika maadili mema na
kuishi katika njia zinazo mpendeza Mungu huku akiwataka kuwalea watoto wao katika maadili ya kumjua Mungu .
Aidha waziri
huyo aliwataka waumini
wa dini ya kislamu tumia kipindi cha mwezi mtukufu wa
ramadhani kumuomba
mwenyezi Mungu kupendana
pamoja na kuvumiliana
“Serikali ya
awamu ya tano ina thamini
mchango wa madhehebu ya dini kila mtu ana haki na uhuru wa kuabudu na kuamini
katika imani yake ya dini hivyo
viongozi wa madhehebu tumieni
majumba yenu ya ibadaa
kuhubiri amani na kuliombea Taifa”alisema
majaliwa .
Mwenyekiti wa umoja
wa madhehebu ya dini mbalimbili Mkoani
humo ( INTER FAITH ) Askofu
Mussa Magwesela akitoa salamu
za umoja huo alimpongeza Rais
Magufuli pamoja na makamu wa Rais Samia Hassani
Suluhu na waziri mkuu kwa
utendaji wao wa kazi kwa kipindi
cha miezi kumi na nane tangu waingie madarakani .
Shekhe mkuu wa mkoa wa Geita Alihaji
Yusufu Kabaju aliwataka waumini wa kislamu na jamii kwa jumla kumuomb Mungu
na kudumisha amani
na upendo .
Awali katibu
wa baraza la bakwata wilayani Chato Shekh Ally
Motondi akisoma risala mbele ya waziri mkuu alisema kuwa asiyeshukuru mazuri
ata kwa Mungu hawezi
kushukuru huku akimpongeza Dk Rais
Magufuli kwa kwa futari hiyo .
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: