Serikali
wilaya ya Geita kufikisha nishati ya
Umeme katika Kitongoji cha Nyamutondo kijiji na kata ya Kaseme kabla ya Mwezi Oktoba mwaka huu ili
kuwezesha Pampu za visima vya maji kutumia Umeme na kusambaza maji kuwafikia
wananchi kwa urahisi zaidi.
Hatua hiyo ya Serikali imekuja ni baada ya
Kukamilika kwa Ujenzi wa Visima viwili kati ya vinne ambavyo vimechimbwa na
wawekezaji wa mgodi wa dhahahu wa Nyamutondo uliopo Kijiji hicho ambavyo
vimejengwa kwa gharama ya shilingi Milioni hamsini na nne (54).
Akizindua
visima hivyo na Kukabidhi kwa serikali ya Kijiji Mwl.Herman Kapufi ,amesema uwezo
wa kusukuma maji kwa sasa katika visima hivyo ni mdogo kutokana na pampu ambazo
wananchi wanazitumia kwa mikono na kwamba kupatikana kwa nishati ya umeme
kutarahisisha na kuboresha huduma ya maji
“Kazi yangu
ni kuhakikisha umeme unaletwa hapa ili kurahisisha swala la maji na kufikia
mwezi wa Kumi umeme utakuwa umefika kwenye kijiji hiki”Alisema Kapufi.
Naye
Mkurugenzi wa Mgodi wa dhahabu wa Nyamutondo Bw.Martin Benda Kajoro amesema
kukamilika na kuzinduliwa kwa visima hivyo kutaondoa changamoto ya maji kwa
wananchi iliyopelekea kufungwa kwa shughuli za uchimbaji wa dhahabu kushinikiza
wawekezaji kuchimba visima.
“Kweli kulikuwa
na shida kubwa sana ya maji lakini kutokana na hali hiyo Mkuu wa wilaya
alituagiza kujenga visima virefu vya maji na sisi tulitilia maanani agizo lake
na ndio maana leo (jana) tumemaliza na tumekabidhi kwake hivyo tunamwomba tu
afikishe kwa afisa madini aweze kutufungulia mgodi wetu maana kwa sasa
hatufanyi shughuli zozote”Alisema Kajoro
Baadhi ya
wananchi wa kijiji hicho ambao wamezungumza na mtandao wa maduka online ,Semeni
John na Koku Gerevasi wamesema walikuwa wakikabiliana na changamoto ya kukaa
kwenye foleni kwa muda mrefu na wakati mwingine kujikuta wakikabiliana na
vurugu.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: