NAIBU WAZIRI KALEMANI"MAMENEJA TANESCO MSIKAE OFISNI WAFUATENI WATEJA"

Share it:
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk Medard Kalemani akizindua mradi wa Umeme Vijijini awamu ya tatu katika Kijiji cha Nyijundu Wilaya ya Nyangh'hwale Mkoani Geita. 



Mkuu wa Wilaya ya Chato,Shaaban Ntarambe akizungumza na kujitambulisha kwa wananchi wakati wa shughuli ya uzinduzi wa umeme vijiji awamu ya tatu.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,akiwasalimia wananchi na kuelezea malengo na manufaa ambayo yatapatikana kutokana na Mradi wa umeme vijijini.

Kifaa cha umeme ambacho kinajulikana  kwa jina la UMETA  kazi yake ni kuraisisha  shughuli ya kusambaza umeme kwenye Nyumba ambazo ni ndogo 

Mbunge wa jimbo la Nyangh'wale Hussein Kasu akipongeza mradi na kusisitiza kuna maeneo ya mradi kwa awamu ya pili kunamaeneo ambayo nguzo zimeanguka Barabara ya kwenda Bukwimba na anaamini Mkandarasi mzuri atachaguliwa awamu hii na kutimiza lengo la mradi kwa faida ya Wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko amewasisitiza wananchi kutumia fursa ya umeme wa REA hususani ni vijana kwaajili ya kujiajiri. 

Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mjini  Constatine Kanyasu ameishukuru Serikali kwa kuweza kusogeza huduma ya umeme vijijini na kuongeza kuwa Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 78.56 kwa ajili ya kugharamia kazi ya usambazaji umeme Mkoani Geita na Wananchi watumie fursa hiyo kwa ajili ya maendeleo yao.

Mkurugenzi mtendaji wa REA Mhandisi  Gissima Nyamo- Hanga amefafanua kuwa kiwango cha upatikanaji wa umeme bado ni changamoto na kuna vijiji 471 na vyenye umeme ni 85 tu sawa na asilimia 18 na mradi ukikamilika jumla ya Vijiji 305 vitakua na Umeme na kuongeza asilimia kufikia 64 hadi kufikia april 2019.

 Meneja Tanesco Kanda ya Ziwa Mhandisi  Amos Maganga ni amesema hivi sasa umeme unaotumika nchi nzima ni Megawati 1000 na mipango iliyopo ni kufikia mwaka 2020 kutakuwa na Megawati 3000.

Katibu wa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Shida Mpondi akimwakilisha Mbunge wa viti maalum Mkoani Humo,ameishukuru Serikali kwa mradi huo na kwamba utaleta maendeleo kwenye jamii na amewataka wananchi kulinda mradi huo.



Naibu waziri wa Nishati na Madini,DR Medadi Kalemani akiwasisitiza wakandarasi wa  shirika la White City  international kutumia miezi kumi na sita(16)Kusambaza Umeme kwenye vijiji  mia  mbili na ishirini (220) ambavyo wamepatiwa  kwenye  Mkoa wa humo.



Naibu Waziri wa Nishati na madini Dk Medard Kalemani akiwapa baadhi Wazee kifaa cha umeme kinachoitwa UMETA(umeme tayari) kama zawadi kwao.




Afisa uhusiano wa Tanesco Mkoa wa Geita Emma Nyaki akimuelezea Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk Medard Kalemani juu ya kifaa cha UMETA kinavyofanya kazi. 

Naibu Waziri wa Madini Dk Medard Kalemani akiwa katika picha na Viongozi na Watendaji mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa TANESCO Mkoani Geita.


Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medard Kalemani amewaagiza Mameneja wa Tanesco wilaya na mikoa yote nchini kuweka madawati kwa ajili ya kuwahudumia wananchi walio mbali na ofisi za Tanesco hususani maeneo ya viijijini.

Amesema wananchi wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma hivyo ni vyema wataalam, meneja na wakurugenzi wakawafuata wateja walipo maeneo ya mbali badala ya kusubiri wafuatwe  ofisini.

“ Na hili ni agizo ninalitoa  kwa nchi nzima mameneja wa Tanesco Ngazi ya Wilaya na Mikoa  wekeni dawati  kwenye maeneo ambayo hayana ofisi za tanesco ”Alisisitiza Kalemani.

Dk Kalemani pia amewasisitiza wakandarasi wa Shirika la White City  International kutumia miezi 16 kusambaza Umeme kwenye vijiji  220 walivyopatiwa mkoani Geita.

Meneja Utaalamu Elekezi wa REA, Mhandisi Gissima Nyamo-hanga amesema katika mradi wa huduma ya umeme vijijini, Serikali imetenga Sh Bilioni 78.56 kwa ajili ya kusambaza umeme mkoani Geita na kuwataka wananchi wawe makini na watu wanaoweza kuwalaghai 

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

Share it:

habari

Post A Comment: