Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh,Ummy Mwalimu ,akikagua Chumba cha dharura kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita |
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh,Ummy Mwalimu,akimjulia hali mama ambaye ni mgonjwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa eita |
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh,Ummy Mwalimu ,amezitaka Hospitali zote za Wilaya na Mkoa
kuanzisha Wodi ya Watoto wachanga kwa ajili ya utoaji wa huduma maalum .
Akizungumza
Wakati alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita,Mhe Ummy amesema watoto wote ambao wana siku ishirini na nane
wanatakiwa kupatiwa huduma ambazo ni maalum na zenye ubora.
Na kwamba
Fedha ambazo zimeahidiwa kutolewa na Mheshimiwa Rais Magufuli Milioni Ishirini
(20) ni vyema zikaelekezwa kwenye ujenzi wa wodi ya mtoto kwenye Hospitali
Hiyo.
“Watoto
wachanga ni rahisi sana kupatwa na magonjwa ya kuambukiza hivyo ni vyema wakawa
na wodi zao ambazo ni maalum ili kusaidia kupatiwa huduma ambazo zinaendana na
umri walio nao hivyo naagiza Hospitali za Mikoa na Wilaya kujenga Hodi za
watoto”
Aidha Waziri
Ummy amekiri kuwepo kwa changamoto kubwa ya wahudumu wa afya kwenye Hospitali
hiyo na kwamba wana mpango wa kuajiri watumishi wa afya elfu tatu (3,000) kwa ajili
ya kuziba mapengo kwa watumishi ambao walikuwa na vyeti Feki.
Mbunge wa
Jimbo la Geita Mjini,Constatine Kanyasu,amemweleza Waziri kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wagonjwa wakilalamikia kuwepo kwa majibu
mabaya kutoka kwa wahudumu ambao wapo kwenye Hospitali hiyo.
“Mheshimiwa
Waziri wagonjwa wengi ambao umewauliza walikuwa wanakwambia huduma ni nzuri ni
kutokana na kuwa na uoga mara nyingi nimekuwa nikipigiwa simu wagonjwa
wanalalamika baadhi ya manesi wana majibu mabaya kwa wagonjwa na hata mganga
mkuu huwa nampigia simu mara kwa mara juu ya malalamiko ya wagonjwa”Alisema
Kanyasu.
Kutokana na
malalamiko hayo Mheshimiwa Ummy
amemwagiza Mkuu wa Mkoa pamoja na Mganga Mkuu kuyafanyia kazi maelezo ya
Mbunge.
Waziri Ummy
amefanya ziara ya kutembelea Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa ikiwa ni utaratibu wake wa kuzunguka kwenye Hospitali na kujionea
huduma ambazo zinatolewa.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: