WAZIRI WA JPM AMWOGOPA MSUKUMA BUNGENI.

Share it:
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Ummy Mwalimu,akizungumza na Wananchi wa Nzera wakati wa kukipandisha rasmi kituo cha Afya Nzera hapo jana na kuwa hospitali ya Wilaya ya Geita.
Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini Joseph Kasheku Msukuma akizungumza na wananchi wa Nzera,.

Wananchi wakisikiliza maelezo ambayo yalikuwa yakitolewa na Mbunge wa Geita Vijijini.




‘’Hivi naweza kutafuta bifu na Msukuma…hivi akikuomba kitu unamkatalia huyu, maana huo mziki wake Bungeni sijui kama nitauweza, zilikuja gari za kubeba wagonjwa sikuweza kumyima….sio kwamba nilimpa kwa kumpendelea nimempa kwa kutambua changamoto za wananzera”.

Ni kauli ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Ummy Mwalimu wakati akikipandisha rasmi kituo cha Afya Nzera hapo jana na kuwa hospitali ya Wilaya ya Geita.

Uamuzi huo wa Ummy Mwalimu unakuja kufuatia ombi la Mbunge wa Geita, Joseph Kasheku Msukuma kumpigia magoti Waziri huyo kwa niaba ya wananchi wa Nzera na Tarafa ya Bugando kwa ujumla kutokana na changamoto zianazowakabili wakazi wa ukanda huo.

Waziri Ummy alisema kuwa amepewa mamlaka makubwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kusimamia sekta ya afya, ambapo ametamba kwamba kuna baadhi ya mambo hasubiri kuomba kutoka kwa Mkuu wa nchi.

‘’Kwa kuwa tarafa ya bugando ina watu laki tatu na themanini na kwa kuwa miundombinu ya hapa inaridhishwa isipokuwa majengo mawili na Mhe. Rais amenipa mamlaka makubwa ya kusimamia sekta ya afya kuna mambo mengine wala sisubiri kuomba kwa rais kwahiyo nimeamua kuanzia leo (jana) kituo cha afya Nzera nakipandisha hadhi kuwa hospitali ya wilaya ya Geita’’alisema Waziri huyo.

Alisema anafanya maamuzi hayo kwa kutambua kuwa wananchi wa Nzera wanayo haki ya kupata hospitali ya Wilaya, ambapo itawaondolea kero ya kusafiri umbali wa kilomita zipatazo 42 kwenda katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Geita.

‘’Kwa hiyo mganga mkuu wa wilaya kazi ni kwako ukiniletea mapendekezo hata kesho mimi natoa hati rasmini ya kimaandishi lakini angalizo langu kwako mwenyekiti wa halmashauri hakikisheni majengo hayo mawili mortuary, thearther mnayakamilisha mapema inavyotakiwa’’alisisitiza Ummy Mwalimu.
MBUNGE MSUKUMA.
Awali Mbunge Msukuma alilazimika kupiga magoti mbele ya wananchi akiomba huruma ya waziri Ummy kukibariki kituo hicho kuwa hospitali ya wilaya kwa kile alichodai kuwa wananchi wake ambao wanakipato duni hawawezi kumudu kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma ya matibabu hususani wazee na wajawazito.

Mhe. Waziri wananchi hawa unaowaona ni wakulima, mpaka wauze mahindi, wakavue dagaa au wauze Ng’ombe ndiyo wapate hela ya kusafirisha wagonjwa sasa wanapopata matatizo ya ghafula usiku kuna vifo vingi sana vya akina mama na watoto,’’

‘’tunakuomba Mhe. Waziri na kwakuwa kauli ya rais ni wanyonge kwanza watu wa jimbo langu ni wanyonge kwelikweli…mama yetu Ummy Mwalimu tunakuomba utamke neon,’’aliomba Mbunge Msukuma.

WAKAZI WA NZERA.

Mzee Paulo Gakala ni Mkazi wa kata ya Nzera hakusita kuelezea hisia zake baada ya Waziri Ummy kuutangazia umma wa wananchi wa Nzera kuwa kituo chao cha afya sasa ni hosiptali kamili, ambapo anasema watu wengi wamefia njiani wakipelekwa katika hospitali ya Mkoa.

‘’wananchi wote tumemuunga mkono waziri ni kweli kwamba changamoto nyingi zitapungua kwa kuwa na hospitali hapa na tunaamini serikali itatuletea madakitari wa kutosha,’’alisema Gakala.

Waziri Ummy alimaliza ziara yake Mkoani Geita kwa kuacha maagizo mbalimbali ikiwemo marufuku aliyoitoa kwa watumishi wa afya kuwatoza fedha akina mama wajawazito waliojifungulia Nyumbani na njiani.

KWA HISANI YA EMMANUEL IBRAHIMU
Share it:

habari

Post A Comment: