Moja kati ya shimo ambapo shughuli za uchimbaji wa madini ukiendelea kwenye mgodi wa Busolwa uliopo kata ya Nyarugusu Wilayani na Mkoani Geita. |
Mkurugenzi wa Busolwa Baraka Ezekiel Nyandu akiwa na Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati alipotembelea Mgodi huo na kujionea shughuli za uzalishaji madini ya dhahabu zikiendelea. |
Mitambo ya kuchenjulia dhahabu kwenye mgodi wa Busolwa. |
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akipatiwa maelekezo na moja kati ya wataalam wa mgodi wa Busolwa namna ambavyo mtambo wa kuchenjua dhahabu umekuwa ukifanya kazi. |
Msafara ukiwa kwenye eneo la kumwagia maji machafu kwenye Mgodi wa Busolwa. |
Bwawa la kumwagia maji machafu ndani ya mgodi wa Busolwa. |
Waziri wa madini Angellah Kairuki akitoka ndani ya mgodi wa Busolwa akiwa ameongozana na Mwenyekit wa chama cha mapinduzi Mkoani Geita,Joseph Kasheku Msukuma. |
PICHA NA MADUKA ONLINE.
Kampuni ya
uchimbaji madini ya dhabau ya Busolwa
imemuomba waziri wa Madini, Angellah Kairuki kuwaongezea eneo la ukubwa wa
kilomita 3.0 kutoka eneo jirani la uchimbaji ili kuweza kuongeza ufanisi zaidi
kwenye shughuli za uchimbaji.
Hayo
yameelezwa na meneja uzalishaji wa Mgodi huo, Felix Aldof wakati wa ziara ya Waziri wa madini na naibu
wake, ambapo alisema kuwa udogo wa eneo
la kufanyia kazi ni sababu kubwa kwa baadhi ya wachimbaji wadogo kuingia kwenye
mgodi huo hali inayohatarisha shughuli za uchimbaji madini.
“Kampuni ya
busolwa mining inayomiliki leseni namba ML 531/2014 inaomba iongezewe eneo la
ukubwa wa kilomita za mraba 3.0 kutoka
eneo jirani na eneo letu la uchimbaji ili tuweze kuongeza ufanisi zaidi
ifikishe ukubwa wa kilomita za mraba 3.53”Aliomba Felix.
Kutokana na
maombi hayo Naibu waziri wa madini,Stanslaus
Haroon Nyongo,ameupongeza mgodi huo kutokana na uzalendo na kumilikiwa
na watanzania huku akiwataka kuendelea na moyo wa kujitolea na kwamba utakuwa
ni mgodi wa mfano kwa wengine kutokana na shughuli ambazo unafanya ikiwemo kusaidia
jamii inayouzunguka.
Aidha kwa
upande wake Waziri wa madini Angellah Kairuki ,ameahidi kushughulikia maombi
yao na kwamba wawaachie nafasi wakaae ili wataalam waweze kupitia maombi hayo
na muda sio mrefu watawarudishia majibu.
Pamoja na
hayo ameushukuru Mgodi huo kwa kuajiri asilimia tisini na tisa ambao ni
Watanzania na mchango ambao wameutoa zaidi ya Tsh Bilion 9.5 ambazo zimelipwa kwa serikali kama kodi
na tozo mbalimbali.
Post A Comment: