Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Aikael Mbowe,
amemkaribisha aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu CCM , Lazaro Nyalandu baada ya kuweka wazi matamanio
yake wapi pa kwenda baada ya kujiuzulu.
Mwenyekiti
Mbowe ametoa fursa ya kumkaribisha ndani ya chama hicho Mhe. Nyalandu
kupitia ukurasa wake wa Twitter na kumwambia kuwa hata masuala
aliyoyaibua yalikuwa ni ajenda ya chama chao kwa muda mrefu.
"Milango iko wazi kwako Lazaro Nyalandu kujiunga na CHADEMA. Masuala uliyoyaibua yamekuwa ajenda yetu kuu kwa muda mrefu" ameandika Mh. Mbowe.
Mh.
Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu CCM jana alitangaza kujiuzulu nafasi zake hizo kwa kile
alichodai kwamba hafurahishwi na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini
na kuwaomba wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama
wataridhia wampe nafasi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kisiasa na
kiuchumi kupitia chama hicho.
Freeman MboweVerified account @freemanmbowetz
Milango iko wazi kwako @LazaroNyalandu kujiunga na CHADEMA. Masuala uliyoyaibua yamekuwa ajenda yetu kuu kwa muda mrefu.
Post A Comment: