VICTORIA FOUNDATION YAKABIDHI MSAADA WA KADI ZA BIMA YA AFYA KWA WAKINAMAMA WAJANE 100 MKOANI GEITA.

Share it:
Mkurugenzi wa Viktoria Faundation  Vicky Kamata pamoja na afisa matekelezo wa mfuko wa bima ya afya Mkoani Geita,Paul Bulolo  wakimkabidhi kadi ya matibabu moja kati ya wakina mama ambao ni wajane wakati wa hafla ya kukabidhi kadi za bima ya afya.

Mkurugenzi wa Viktoria Faundation  Vicky Kamata akielezea madhumuni ya taasisi hiyo kutoa msaada wa kadi za matibabu.

Moja kati ya wakina mama ambao ni wajane akifurahia baada ya kupatiwa kadi ya matibabu.

afisa matekelezo wa mfuko wa bima ya afya Mkoani Geita,Paul Bulolo  akitoa elimu ya matumizi ya kadi ya bima ya afya wakati wa shughuli ya kuwakabidhi wakina mama  wajane mia moja.
Mkurugenzi wa Viktoria Faundation  Vicky Kamata akifurahia na kuburudika na wakina mama wajane ambao wamepatiwa kadi za matibabu. (picha na Maduka Online)


NA JOEL MADUKA.




Taasisi isiyo ya kiserikali ya Victoria Foundation imetoa msaada wa kadi za bima ya afya kwa wakina mama wajane mia moja(100)Mkoani Geita.


Akikabidhi Kadi hizo mapema leo  Mkurugenzi  wa  taasisi hiyo ambaye pia ni mbunge wa viti maalum Mkoani humo kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM)  Vicky Kamata alisema  kuwa wameonelea  ni vyema wakatoa msaada wa bima za afya kwa wakina mama wajane kutokana na adha  ambazo wamekuwa wakikutana nazo na kwamba kundi hilo limesahaulika sana na wengi wao wanakuwa  hawana uwezo wa kujikimu gharama za matibabu pindi wanapokuwa wameugua.


“Wakina mama wajane tumeamua kuwasaidia bima za afya kutokana na wengi wao wamekuwa awana uwezo wa kufanya shughuli ambazo zinaweza kuwasaidia kiuchumi na wengine unakuta hata gharama za matibabu kwao ni tatizo hivyo sisi tumeonelea kwa awamu hii ya kwanza tuanze na wakina mama mia moja kasha tutaendelea na awamu nyingine tena”Alisema Kamata.


Pia ameongezea kuwa jumla ya kiasi cha fedha ambacho kimetumika kugharamia kadi hizo za bima ya afya ni Milioni saba na laki sita.


Kwa upande wake afisa matekelezo wa mfuko wa bima ya afya Mkoani Geita,Paul Bulolo alisema pamoja na kutoa kadi hizo kwa wakina mama lakini pia wamewaomba kutengeneza vikundi vya ujasiriamali ambavyo vitawasaidia kujikwamua kiuchumi hali ambayo itawasaidia kuhuisha kwa mala nyingine kadi  za bima ambazo wamepatiwa siku ya leo.


“Kadi hii ya bima ya afya itakusaidia kutibiwa sehemu yoyote na maeneo yoyote hapa nchini na hivyo basi tunajua kuwa kadi hizi zinamwaka mmoja nilikuwa nawaomba wakinamama kutumia fursa hii kuunda vikundi vya ujasirimali ambavyo vitawasaidia kuhuisha kadi zenu pindi zinapokuwa zimemaliza muda wake”Alisisitiza Bulolo.


Bi,Maneshu Lema ni moja kati ya wakinamama ambao wamenufaika na kupatiwa kadi ya bima ya afya pamoja na kushukuru taasisi hiyo alisema kuwa miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakikutana na changamoto ni pamoja na wajane  na kwasasa wamesaidiwa kwa kiasi kikubwa kwani hawatakuwa na mawazo ya gharama za  kutibiwa .


Share it:

habari

Post A Comment: