mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anacheza ngoma ya kimasai pamoja na baadhi ya wamasai waliojitokeza katika sherehe za kupandisha ngazi ya rika kutoka katika rika la kurianga kuingia katika rika la Nyangulo (habari picha na woindeshizza blog )
mbunge akiwa na wananchi waliouthuria katika sherehe hizo
mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anasalimia na moja na mzee aliekuwa rrika la kurianga ambae kwa sasa ameingia katika rika la Nyangulo
Wazazi hususa ni jamii ya kimasai
wametakiwa kuachana na zana ya kuwatenga na kutowapeleka shule watoto wa kike
na wale ambao ni walemavu badala yake
wawapeleke mashuleni kwani wao ndio viongozi wa baadae.
Hayo yamebainishwa na mbunge wa viti
maalumu kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Amina Mollel wakati alipokuwa
akizungumza kama mgeni rasmi katika sherehe za kupandisha ngazi rika kutoka katika rika la kurianga
kuingia katika rika la Nyangulo ,sherehe ambazo zilifanyika katika Kijiji cha
Oldenderet Kata ya Nduruma mkoani Arusha.
Alisema kuwa kunabaadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto wao kisa ni walemavu jambo ambalo
linawakosesha haki zao ikiwemo ya kupata elimu
kutokana na kufichwa huko.
“kwakweli wazazi wanavyoficha watoto wao hususa ni walemavu wanawanyima haki yao mfano kama mimi ningefichwa leo kweli ndugu zangu ningeweza kuwa kiongozi hivyo napenda kuwasihi wazazi wasiwafiche watoto hawa kwani wakiwapeleka shule kupata elimu itakuwa vizuri kwani pale watakapo maliza shule wanakuja kuwasaidia “alisema Amina.
Aidha pia aliwataka wazazi hawa wa jamii ya kimasai na hata wale wa makabila mengine kuacha kuwaozesha watoto wakike mapema kwani watoto hao wakike nao wanahaki ya kupata elimu kwani elimu ni bure ,kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari hivyo ni vyema kama wazazi wakawasimamia watoto hususa ni wakike wakaenda shule.
Aliongeza kwa kuwasihihi watoto wa kike kuweka kipaumbele
swala la elimu kwani elimu ndio kila kitu katika maisha yao na iwapo watasoma
kwa bidii wanaweza kuwa viongozi wakubwa
wa serikalini hapo baadae.
Alisema kuwa kunabaadhi ya watoto wa kike wamekuwa wanaacha
kusoma kisa wanakimbilia maisha kitu ambacho sio kizuri kwani wanaweza
kukimbilia maisha yakawapiga hivyo ni muhimu sana kama watasoma kwanza alafu
maisha watayapata baadae baada ya kumaliza kusoma na kupata kazi zao nzuri.
“napenda kuwasihi ndugu zangu wamasai kuachana na mila za
kizamani kama vile ukeketaji na kuozesha watoto wa kike mapema kwani swala hilo
sio jema na limepitwa na wakati na napenda kuwataka wananchi wote hususa ni
ndugu zangu wamasai kuwafichua wale wote ambao bado wanaendeleza mila za zamani
kama vile ukeketaji”Alisisitiza Amina .
Post A Comment: