Wananchi wa Kijiji cha Senani wakimshuhudia Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Kandege alipokuwa akiweka jiwe la Msingi katika zahanati ya kijiji hicho. |
Ujenzi wa Tanki la Maji katika kijiji cha Ikungulipu wilayani Itilima, alipokuagua Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Josephat
Kandege jana. |
NA
COSTANTINE MATHIAS, ITILIMA.
NAIBU Waziri
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Josephat Kandege amezitaka
Halmashauri zote nchini kufanya manunuzi ya bidhaa bila kutumia wakandarasi (force
account) ili kupunguza gharama za ujenzi wa miradi.
Kandege aliyasema
hayo jana wakati akikagua, kuona na kuweka mawe ya msingi katika ujenzi wa vyumba
vya madarasa, zahanati na mradi wa maji wilayani Itilima mkoani simiyu.
Alisema kuwa
serikali ingependa Halmashauri zitumie force accont ili kupunguza gharama za
ujenzi wa miradi kwa sababu wakandarasi wengi wamekuwa wakipandisha bei ya
bidhaa kuliko uhalisia.
Akisoma
taarifa ya ujenzi wa Nyumba nne za watumishi, Afisa Mipango wilaya ya Itilima
Paulo Nyalaja alisema kuwa nyumba hizo za zitapunguza suala la uhaba uliokuwa
unawakabili watumishi hao.
Alisema kuwa
nyumba hizo zinajengwa na mkandarasi wa kampuni ya Gati Eng. Co. Ltd ambapo zimegharimu
milioni 268 huku kila nyumba ikijengwa kwa milioni 67.
Mbunge wa
Jimbo la itilima Njalu Silanga alisema kuwa katika Jimbo hilo kuna Majengo 28
ya zahanati yaliyofikia hatua ya ukamilishaji kwa nguvu za wananchi na kuitaka
serikali kuunga mkono juhudi za wananchi.
Aliongeza kuwa
shule ya msingi Migato ina uhaba wa vyumba vya madarasa wakati huo ikiwa na
wanafunzi 1933, na kumtaka Naibu waziri kuzipa kipaumbele cha usajili shule shikizi
na shule bubu.
Naibu Waziri
Kandege aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Nyumba za watumishi Itilima, zahanati
Senani, madarasa ya manne ya shule ya msingi migato, kukagua ujenzi wa jengo la
halmashauri, mradi wa maji Itilima Ikungulipu.
Post A Comment: