Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwabalogi Kijiji cha Kifufu ambaye ambaye ametengwa na wananchi kutokana na kugoma kulipa faini ya shilingi laki sita. |
Diwani wa kata ya Bugalama , Luponya Masalu akiwasisitiza wananchi kuishi kwa amani na kusameheana makosa yao ili kuruhusu maendeleo kwenye Kijiji cha Kifufu. |
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Diwani wakati alipokuwa akihutubia hadhara hiyo. |
Wakina Mama wakifuatilia Mkutano huo. |
Meza kuu ikiongozwa na Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa kikao hicho. |
Wananchi wa Kijiji cha Kifufu Kata ya
Bugalama Wilayani Geita wameazimia kumtoza faini ya shilingi laki sita Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwabalogi kutokana
na kuwepo kwa tabia ya watoto wake kuingia kwenye makazi ya wanakijiji na kuiba
mifugo pamoja na mazao.
Hata hivyo mwenyekiti huyo Bw Nchemba
Kasomeko amesababisha hali ya sintofahamu kwa wanakijiji baada ya kugoma kuomba
msamaha na kukiri makosa ambayo yamesababishwa na watoto wake mbele ya mkutano
wa hadhara ulioitishwa na diwani wa kata hiyo uliokuwa na lengo la kuleta
suluhu baina yake na wanakijiji kutokana na tuhuma za kuwahifadhi wahalifu
wakiwemo wajukuu zake jambo ambalo limesababisha uvunjifu wa sheria.
Katika Mkutano huo Bw Nchemba
anadaiwa kuwakejeli wananchi pamoja na viongozi wa kata wakiongozwa na
Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata hiyo baada ya kumtaka alipe faini ya
Sh Laki 6 ya kuhifadhi wahalifu baada ya wajukuu zake kutuhumiwa kwa wizi wa
matikiti maji kwenye shamba la Leonard Martin kwa kuwaita masikini.
“Ndugu zanguni mimi nashangaa watu
kusongamana kila wakati mnanitafuta mimi tu,nimekuwa kama dume la wizi na nyie
viongozi hapa mbele ni wanafiki tu na kitu cha kukaa ninasumbuliwa nitoe laki
sita wakati sio mwizi wizi ni watoto
mliwaachia nyie kuwa mmewasamehee leo tena mnataka nitoe mahela mengi
wanakijiji nilishawai kufika kwako
nikakomba mboga tatizo umasikini wenu unawasumbua au mnataka nitoke humu
nijenge Geita”Alifoka kwenye Mkutano huo.
Kutokana na Majibu ya Nchemba kuwa ya
kejeli na kuto kuafiki kulipa faini ya Sh Laki 6, baadhi ya wananchi
wamechukizwa na kauli zake na kuuomba uongozi wa kijiji na kata kuondoka nae .
“Kweli Nchemba asijione anavyo sana
kuliko wananchi kama kuna faini naomba atoe hiyo faini sio yeye ajifanye anavyo
sana jamani kwani Mungu aliumba Masikini na matajiri”Alisema Getruda Kachwele.
“Ndugu mwenyekiti nadhani Muda
unakwenda na hili la Nchemba hatutalimaliza sisi tulikwisha wapatia mtu wenu
mnaonaje kama mtamchukua muende nae tu maana sisi huyu hatuwezi kuendelea kuwa
na mtu wa namna hii kijijini hapa”Alisikika akisema Musa Msafiri.
Kufuatia madai hayo kwa wananchi
Diwani wa kata Hiyo, Luponya Masalu amemtaka Bw Nchemba kuwaomba radhi wananchi
na kuwalipa wananchi pesa ya faini ambayo anadaiwa lakini amekaidi na kumtaka
diwani kumuacha akajifikirie.
Julai 23 Mwaka huu Mkutano Mkuu wa
Kijiji hicho uliketi na kuazimia Bw, Nchemba alipe kiasi hicho cha fedha ambapo
alikubali lakini leo ameyatupilia mbali maamuzi hayo .
Imeandaliwa na Mtandao wa Maduka Online.
Post A Comment: