NA JOEL MADUKA
Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13ambaye anasoma darasa
la tano Shule ya Msingi Ibondo, Kata ya Rudete, Wilayani Geita, (Jina
tunaliifadhi) amejifungua kabla ya
wakati katika choo cha shule baada ya kupata uchungu wa ghafla.
Hali hiyo ilizua taharuki
miongoni mwa wanafunzi na walimu shuleni hapo ambapo mtoto huyo alipokimbilia
chooni baada ya kujisikia haja kubwa na badala yake alitoka mtoto wa umri wa
kati ya miezi 4hadi 5.
Akisimulia mkasa huo, Mwanafunzi
huyo alisema kuwa muhusika wa ujauzito huo ni kijana mkaazi wa kijiji hicho
ajulikanaye kama Laurent Ngasa, alisema siku ya tukio alikuwa hayupo vizuri kwani alipata maumivu ya kichwa,na baadaye wakati
masomo yakiendelea alijisikia kupata haja kubwa na alipokwenda chooni ndipo
hali hiyo ilipomtokea.
“Nilipofika chooni nilisikia kitu kinatoka
kumbe ni mtoto nilipatwa na hofu nikakimbilia nje nyuma ya moja ya madarasa
nikachuchumaa na ndipo kikatoka tena kitu kingine sasa hapo ndipo wanafunzi
wenzangu wakakimbila kuwaambia waalimu,”alisema Mwanafunzi huyo.
Aliwezaje kuhudhuria masomo kwa miezi
kwa miezi hiyo yote bila kugundulika.
Baada ya kuhojiwa kuwa aliwezaje
kuficha ujauzito huo bila wazazi na walimu kumtambua kuwa ni mjamzito, alisema walimu na wanafunzi wenzake walikuwa
wakimuuliza kuwa kwa nini ana tumbo kubwa lakini hakuna aliyehisi kuwa ni
mjamzito.
“Kuna siku moja mwalimu mmoja
aliniita mara tu baada ya kupata chakula cha mchana, akaniuliza mbona tumbo
lako kubwa sana, nikamjibu kuwa nilikula wali mwingi,”alisema.
Akizungumzia kuhusu hali ya mtoto
huyo, baba wa mwanafunzi huyo, Wiliam Bukwimba, alikanusha kuwa na taarifa wala
kuhisi kuwa mtoto wake ni mjamzito katika kipindi chote cha ujauzito huo.
“Kusema kweli sikuwahi kumgundua
huyu mwanangu kuwa ana ujauzito na kila siku alikuwa akihudhuria masomo yake
kama kawaida,”alisema.
Naye rafiki wa Mwanafunzi huyo,
aliyejitambulisha kama Rebeka Ades, ambaye wanakaa dawati moja, naye pia
alikanusha kujua wala kuhisi kuwa rafiki yake huyo ana ujauzito.
Alisema kuna siku walikuwa pamoja
wakipata chakula cha mchana ambapo mwalimu alimwita na kumuuliza kwa nini
amekuwa na tumbo kubwa sana na akamjibu kuwa ameshiba sana.
“Hata wakati wa kipindi cha michezo,
alikuwa anatabia ya kukaa pembeni huku
akionekana na mawazo mengi tulikuwa tukimcheka sana kuhusu tumbo lake lakini
hatukujua kuwa ni mimba,”alisema.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata
ya Rudete, Sebastian Benedicto alisema tukio hilo ni la kusikitisha sana na
kwamba ni lazima muhusika wa ujauzito huo achukuliwe hatua kali za kisheria.
Aidha, alisema alipata taarifa ya
tukio hilo wakati wa ziara yake kwenye kata hiyo ambapo alitembelea maeneo
mbalimbali ya huduma za kijamii zikiwemo shule, zahanati na kuangalia
changamoto zilizopo katani mwake.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka
katika zahanati ya kijiji hicho, wahudumu walifanikiwa kumfanyia vipimo na
kujidhihirisha kuwa alikuwa na ujauzito.
.
Akifafanua juu ya hali ya usalama
wa mtoto huyo, muhudumu wa Zahanati ya Ibondo, Aloyce Aron, alisema walimpokea
mtoto huyo saa 7.30 mchana ambapo vipimo vilionyesha kuwa alikuwa na mimba ya
umri kati ya miezi 4-5.
Post A Comment: