Waziri mkuu wa Uturuki akisalimiana na watanzania |
Wafanyabishara wa kitanzania walioshiriki kongamano. |
Waziri mkuu akihutubia. |
Waziri mkuu wa wa
Uturuki Binal Yildirim
amempongeza Ras John Pombe
Magufuli na Watanzania wote
kwa kudumisha ushirikiano wa Nchi hizo mbili na
kuahidi kuendelea kuulinda kwa
manufaa ya Nchi zote mbili.
Amezungumza hayo kwenye
ufunguzi wa kongamano kubwa la kibiashara lijulikanalo
kwa jina la
Turkish Exporter’s Assembly
Week, lililofanyika kwenye ukumbi wa
Istnbul Confress Center na
kuhudhuriwa na wafanyabishara
zaidi ya 1000 kutoka
Nchi mbalimbali Duniani.
Yildirim alisema kuwa,
Rais John Pombe
Magufuli ameonyesha nia ya
Tanzania na Uturuki kufanya kazi ka pamoja kwa manufaa ya raia wa Nchi
hizo mbili, hivyo ni suala
la kupongezwa kwani lina faida
kubwa kwenye ukuaji wa
uchumi kwa Nchi
hizo mbili.
Pia amewapongeza watanzania kwa kuwa
na historia nzuri ya
ukarimu na kusisitiza kuwa,
wafanyabisha wachangamkie fursa
za kibishara kwani Uturuki
ipo tayari kufanya
biashara na Tanzania,
kutokana na Tanzania kuwa na bidhaa
nyingi zenye uhitaji mkubwa Uturuki, na
pia Uturuki ina uwezo wa kiteknonolojia na
inaweza kusaidia falsafa ya uchumi wa
viwanda kwa Tanzania.
Mfanyabishara wa Tanzania
Abuu
Kondo , alisema kuwa kongmano
hilo limemsaidia kupata wafanyabishara wapya
wa Uturuki ambao wengi wameonyesha
nia ya kushirikiana na watanzania kwenye Nyanja mbalimbali
za kibiashara, hivyo lina mchango
mkubwa kwa ukuaji wa biashara
yake.
Naye Balozi wa
Tanzania Nchini Uturuki
Elizebert Kihondo, alisema
kuwa, kongamano hilo lina
fursa kubwa kwa
wafanyabishara wa kitanzania, kwa
kuwa linawakutanisha wafanyabishra wa Nchi
mbalimbali na wnaweza kushirikiana
katika kuhimiza ujengwaji
wa viwanda Nchini na kusukuma
mbele ukuaji wa uchumi wa viwanda.
“Unajua wenzetu Uturuki wamekuwa na
uzoefu sana kwenye Nyanja ya viwanda hivyo basi
tukiwatumia vyema wanaweza
kwenda nyumbani kama wawekezaji na kujenga viwanda” alisems balozi Kihondo.
Naye Makamu wa rais
wa chama cha
wafanyabiashara wa viwanda
na kilimo Tanzania bwana Octavian
Mshiu alisema kuwa, wafanyabishara zaidi
ya ishirini toka
Tanzania wamepata nafasi ya
kuja kwenye kongamano hilo ni matumaini
yake kuwa watashiriki kikamlifu
kwenye kupanua mahusiano na
uwekezaji wa kibishara kwa kushirikiana na
wenzao wa uturuki .
“Sisi kama chama
tutahakikisha tunazidi
kutengeneza fursa nyingi
kwa wanachama wetu za kupata
nafasi za kujifunza uwekezaji
kupitia mahusiano tuliyonayo
na Nchi ya
Uturuki pamoja na
Nchi mbalimbali Duniani” Alisema
Mshiu
Pia wafanyabiashara wa
Tanzania wao ndio
pekee waliopata naafsi
ya kuongea na waziri
mkuu na kumkabidhi
zawadi za kiasili vikiwemo ninyago
kutoka Tanzania.
Historia
inaonyesha Nchi ya
Uturuki na Tanzania zina mahusiano mazuri
kwenye Nyanja za kiuchumi hasa
katika utekelezaji wa miradi mbalimbali
ya kimaendeleo ukiwemo wa
ujenzi wa reli ya
kisasa kutoka Dar es
Salaam kwenda Morogoro.
Post A Comment: