" Wananchi wanatakiwa
kusimamiwa ata kama fedha ni za kwao ili kuweka miradi katika ubora
unaotakiwa"Alisisitiza Lughumbi.
Aidha, alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato kuhakikisha
wananchi wanakuwa katika vikundi ili vishiriki katika ujenzi na utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo katika vijiji kwa kuchangia michango midogo
midogo kama vile kutafuta mawe, kokoto, mchanga. Kazi kubwa ya Halmashauri ni kuhakikisha wahandisi
wanasaidia kupeleka michoro na kusimamia ujenzi wa miradi ya Zahanati na
madarasa katika vijiji husika.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Chato
kufuatilia ujenzi wa Bweni la wanafunzi shule ya Sekondari Jikomboe ambalo
limegharimu kiasi cha Shilingi milioni 75 ili kujiridhisha kama fedha hizo
zimetumika kama ilivyokusudiwa na kuona kama thamani yake inaonekana.
Akiwa Wilayani Chato Mheshimiwa Robert Gabriel ametembelea shule ya
Msingi Chato na kukagua ujenzi wa vyumba
vya madarasa sita na vyoo, ujenzi wa Zahanati ya kijiji Mganza, ujenzi wa Bweni
shule ya Sekondari Zakia Meghj pamoja na Ujenzi wa Soko la dagaa Kasenda na
kuagiza takukuru kufika katika miradi hiyo ili kufuatilia matumizi ya fedha
katika miradi ya Zahanati, Bweni na madarasa.
Vilevile Mkuu wa Mkoa ametembelea ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato na
kupongeza jitihada za utekelezaji wa mradi huo zinazoendelea kwa kufikia
asilimia 63. Awali Meneja wa Tanroads Mkoa wa Geita Mhandisi Haruna Senkuku
alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa uwanja huo una Run way ya Kilometa 3 ambapo hadi
kukamilika mradi utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 39.
Post A Comment: