Kiongozi wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Mh.
Zitto Kabwe amesema watafungua kesi mahakamani kupinga baadhi ya
vifungu vilivyomo katika Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 ambayo amedai
inanyima uhuru wa wananchi kuchambua takwimu.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya kitengo cha
upelelezi wa makosa ya kifedha kilichopo Kamata, Kariakoo jijini Dar es
Salaam, Zitto amesema haiwezekani kukawa na mamlaka moja ya kutoa
takwimu.
"Tunataka kufungua kesi mahakamani kupinga sheria ya
takwimu kuzuia watu kuchambua, huko ndiko ukweli utajulikana na wananchi
watajua sheria hii ilivyo. Hii itakuwa kesi ya kwanza kwa sheria hii
kupelekwa mahakamani," amesema Zitto.
Amesema, "Tuna taarifa ambazo hatukuzitoa, tukifika
mahakamani tutazitoa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu haiwezi kusema una
hatia au la kwa kuwa wao si Mahakama. Tungefurahi kama jambo hili
lingekwenda mahakamani" Zitto
Ameongeza kwamba "Sisi tulitumia takwimu zao kuchambua na tumewaeleza polisi kwamba tutawaeleza zaidi tukifika mahakamani."
Kuhusu tuhuma za uchochezi zinazomkabili Mh. Zitto
amesema kwamba , “Nimeripoti leo kama nilivyotakiwa lakini nimeelezwa
nirudi tena Ijumaa Novemba 17, 2017 wanadai wanasubiri chaji kutoka kwa
Mkurugenzi wa Mashtakana baada ya hapo wataona kama watanipeleka
mahakamani au la.''
Hata hivyo Kiongozi huyo ambaye ni Mbunge wa Kigoma
Mjini amesema kwamba kesho atarudi tena kituoni hapo tena kesho muda wa
asubuhi kwakuwa anatuhumiwa kwa kesi mbili ya sheria ya takwimu na
makosa ya mitandao.
Post A Comment: