Gari aina ya
Scania lori lenye namba za usajili T415
DJG limechomwa moto baada ya kumgonga
mwendesha pikipiki na kusababisha kifo cha Matha Paulo aliyekuwa ni Muuguzi wa kituo
cha afya cha Kaseme Wilayani Geita alikuwa amebebwa kwenye pikipiki hiyo.
Tukio hilo
limetokea majira ya saa moja jioni katika kijiji cha Kasesa kwenye barabara ya
katoro-Lunzewe ambapo mwendesha boda boda na abiria wake walikuwa wakitokea mji
mdogo wa Katoro,huku watoto wawili akiwemo kichanga cha miezi miwili (2) waliokuwa
wamepakatwa na marehemu mama yao wakinusurika kifo.
Akisimulia
shuhuda wa tukio hilo Bw,Mayala Bushibe, alisema yeye alikuwa ameongozana na
boda boda iliyopata ajali,huku nyuma na mbele yao yalikuwapo magari mawili
likiwemo lori yakipishana na mwendesha piki piki alipojaribu kulipita ndipo
likawagonga gari hilo.
“Baada ya
utelezi wa mvua akayumba Yule dereva wa
boda boda akaanguka na gari la nyuma likampitia ikabidi akimbie Yule boda boda
na baada ya kuangalia Yule mtu aliyegongwa tulijua ni nesi wa kaseme”Alisema
Mayala.
Josia
Thobias ambaye ni mkazi wa Kaseme alisema
tukio la namna hiyo sio la mara ya kwanza kutokea kwani ajali za hivyo zimeendelea kujitokeza na
kwamba ni mara ya pili kutokea.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Geita Mponjoli mwambulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kusema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa pikipiki ambaye alikimbia
baada ya kutokea kwa ajali,huku akiwataka wananchi kuachana na vitendo vya
kujichukulia sheria mkononi.
Post A Comment: