WATU 15 WANASHIKIRIWA KWA TUHUMA ZA UNYANG'ANYI MKOANI GEITA

Share it:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Akizungumza na waandishi  juu ya msako ambao wamefanya na kukamata vwaharifu 15.
Vitu ambavyo avijatambuliwa.

Moja kati ya watu ambao wanasadikika kuiba kwenye duka la Nguo akiwa amepigwa na wananchi.



Na,Joel Maduka,Geita.

Vitendo vya uhalifu Mkoani Geita , vikiwemo vya uporaji wa simu na vitu vya ndani kama Televisheni na Redio  vimezidi kukithiri ambapo Jeshi la Polisi hadi sasa linawashikiliwa watu 15 kutokana na vitendo hivyo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema kutokana na msako walioufanya  tarehe 28 February Mwaka huu hadi March 6 mwaka wamewakamata watuhumiwa na vitu mbalimbali.

Kamanda Mponjoli alisema vitu ambavyo hadi sasa havitajatambuliwa ni  televisheni Sita(6) , Redio mbili(2) za Sub woofer, Spika mbili (2)na simu Nne(4) pamoja na Deki moja (1).

“Vitu ambavyo havijatambuliwa hadi sasa ni Televisheni flat screen LG nchi 42, televisheni flat screen home base nchi 24, Televisheni flat screen aborder nchi 49, televisheni flat screen aborder nchi19, televisheni flat screen tandar 19, televisheni flat screen Mobisol nchi 19,Sub woofer aborder 1,Sub woofer Seaoeano 1, Simu ya Tecno W4, Tecno C8, Tecno Boom J8, Blackberry Q10, Laptop HP 1,DVD Deck 1”alisema Kamanda Mponjoli.

Kamanda Mponjoli ametaja tukio jingine ni la Bw Charles Masangwa ambaye aliuawa  kwa kupigwa na fimbo kifuani na Mashaka Sinzya  (65)hali iliyosababisha akimbizwe katika kituo cha afya Katoro baada ya maumivu makali kabla ya kufariki

Baadhi ya wananchi Mkoani humo wameendelea kusikitishwa na vitendo vya wizi kukithiri hali inayosababisha hali tete ya kiusalama kwenye makazi ya watu

Hata hivyo Kamanda Mponjoli ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kujitokeza kwa ajili ya kutambua vitu vyao.


Share it:

matukio

Post A Comment: