Baadhi ya wachimbaji wadogo wakifuatilia mafunzo ambayo yalikuwa yanatolewa na wakala wa afya na usalama mahari pa kazi na ofisi za Afisa madini Mkoa wa Geita. |
Baadhi ya wachimbaji wadogo wakifuatilia mafunzo ambayo yalikuwa yanatolewa na wakala wa afya na usalama mahari pa kazi na ofisi za Afisa madini Mkoa wa Geita. |
Kaimu meneja wa wakala wa afya na usalama mahari pa kazi Bw,Mjamo Mohamed akisoma taarifa ya semina hiyo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita. |
Kamishina msaidizi wa madini kanda ya ziwa Viktoria Yahaya Samamba akizungumzia juu ya semina hiyo na faida ambazo watazipata wachimbaji kutokana na mafunzo ambayo watapatiwa. |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kwaajili ya kuzungumza na wachimbaji wadogo Mkoani Humo wakati wa semina iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Moyo wa Huruma. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Geita ,Leornad Bugomola akielezea tatizo la Kabon kuendelea kusafirishwa kwenda Jijini Mwanza. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini Mkoani humo. |
NA,MADUKA ONLINE HABARI.
Kipindi cha kuanzia Julai 2017 hadi machi mwaka 2018
wachimbaji wadogo Mkoani Geita wameripotiwa kuzalisha kiasi cha Kg68.55 zenye
thamani ya Sh,Bilioni 6.5 ongezeko hilo la uzalishaji linatokana na marekebisho
ya sheria ya madini ya mwaka 2017 pamoja na kanuni zake za mwaka 2018.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Geita mhandisi Robert
Gabriel wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja yaliyokuwa yamelenga
kuwawezesha wachimbani wadogo kutambua
mbinu za kujikinga na ajali zinazotokana na mvua ambazo zinaendelea Kunyesha.
Mheshiwa Gabriel amesema serikali itaendelea kusimamia na
kukusanya mrabaha na tozo kwa kufuata utaratibu wa sheria ambazo zinawataka
wachimbaji wadogo kulipa tozo kutokana na shughuli ambazo wanazifanya kwenye
maeneo hayo.
Miongoni kati ya mambo ambayo yameonekana ni changamoto ni
usafirishaji wa kaboni ya kuchenjuliana madini ya dhahabu kwenda mwanza
ambapo Mkuu huyo amesema wanatarajia
kutoa matangazo ya kuzuhia shughuli hiyo ya kusafirisha kaboni na kwamba
itatumika ndani ya mkoa huo kutokana na mapato ambayo yameendelea kupotea.
Kamishina msaidizi wa madini kanda ya ziwa Viktoria Yahaya
Samamba amesema mapendekezo hayo ni mazuri na kwamba watakaa na wamiliki wa
makarasha ili waweze kuwashauri kuwa na mashine ambazo zitasaidia wachimbaji
wadogo kutokupeleka kaboni mwanza na shughuli hizo zitakuwa zikifanyika Mkoani
humo.
Aidha kwa upande wake kaimu meneja wa wakala wa afya na usalama mahari pa kazi
Bw,Mjamo Mohamed alisema kuwa wameamua
kukaa na wachimbaji kutoa semina ya kujikinga na majanga kwenye maeneo yao ya
kazi kutokana na mvua ambazo zimeendelea kunyesha hivyo kufanya hivyo
kutawasaidia kuepukana na majanga ambayo yanaweza kusababisha watu kupoteza
Maisha.
Hata kwa kwa upande wa mmoja kati ya wachimbaji wadogo
ambaye amezungumza na mtandao huu,ameishukuru ofisi ya madini mkoani humo
pamoja na wakala wa afya na usalama mahari pa kazi kuendesha semina hiyo na
kwamba imewajenga na pia imewapa mwangaza kwani wametambua namna ambavyo
wanaweza kujikinga na majanga kwenye maeneo yao ya kazi ikiwa ni pamoja na
kuwapima afya watu ambao wanawaajili kwenye shughuli zao.
Post A Comment: